Katiba zetu na wanzungu!!!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba zetu na wanzungu!!!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Aloysius, Jul 21, 2011.

 1. Aloysius

  Aloysius Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mnahabari kuwa pengine hizi kelele za kubadili katiba zinabarikiwa na Wazungu?!!! Vijana tufumbue macho, historia inamueleza mzungu kama mtu wa uchu wakututawala toka enzi kiakili na kwa kila kitu. Ona anachofanya Libya, Ivory Cost, Sudan, Somalia n.k. Kenya ni mfano mdogo; swala la "abortion" lilipenyezwa kwenye katiba pindi tu ilipobadilika ikawaacha wakenya hata wale waliotaka ibadilike midomo wazi, mpaka wakujiuliza hili ni la nani, kura ilikuwa yakusema ndio au hapana. Wakaipitisha kwakuadiwa mabadiliko yatafanyika. Je yamefanywa? Kwetu nini kitapenyezwa?!!!
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Za wazungu kuchimba uranium, dhahabu na kuchukua maelfu ya ardhi yetu mbona huzungumzii wewe unaona hicho cha mabadiliko ya katiba ndo kinauma zaidi kulikowazungu wanavyotuibia waziwazi??????
   
 3. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna cha wazungu hapa, acha ubaguzi.... mzungu ni nani? mtu anaanza kuitwa mzungu akiwa na sifa zipi? wewe hujui kwamba tuna matatizo kibao kwenye Katiba yetu ya sasa yasiyohusu wazungu? madaraka makubwa ya rais kuteua (na kuwafukuza akitaka) majaji, makatibu wakuu, wabunge wa kuteuliwa, makamishina, ma-inspekta, wakurugenzi, ma-DC, nk, na kupuuza maamuzi ya mahakama, kuinglia uhuru na mamlaka ya bunge, katiba inayominya haki za binadamu, ....hayo nayo ni ya wazungu?. Katiba hii tumekuwa tukiililia kwa muda tangu enzi za Mkapa, katiba iliyopo ni ile iliyoachwa na wakoloni tumweka viraka tu. Ukifika wakati wa kupiga kura ya maoni upige kutaka katiba mpya achana na dhana ya uzungu na katiba yetu.
   
 4. Aloysius

  Aloysius Member

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya bwana
   
Loading...