Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Mchakato wa katiba mpya ulikwama. Bado Tanzania ina uhitaji wa Katiba mpya. Kama nchi, ili kupata Katiba mpya mwaka huu au hata ujao, tuanzie wapi ili kusonga mbele?
- Tuanzie kwenye Katiba Inayopendekezwa na kuendesha Kura ya Maoni? Hapa tutahitaji mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazosimamia Kura ya Maoni kwakuwa kisheria, mchakato ulishakwama, yaani, muda wa kufanyika mambo mengi ulishapita.
- Tuanzie kwenye Raismu ya kwanza au ya pili ya Tume ya Jaji Warioba? Hapa patahitajika kuundwa tena kwa Bunge Maalum la Katiba na mjadala kufanyika tena. Mjadala na mchakato utakapokamilika, Katiba Inayopendekezwa itapatikana na kupigiwa kura.
- Tuanzie kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba? Yaani, mchakato wa Katiba mpya uanze upya kabisa?