Katiba mpya Itaandikwa na Vijana Wazalendo

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
37,547
47,200
Kumekuwepo na uhitaji mkubwa mno toka kada mbalimbali kwa umuhimu wa kuwa na katiba mpya itakayokidhi matakwa na mahitaji yaliyopo kwa sasa kulingana na hali ya maisha.

Swala la katiba mpya , itafikia mahali halitaepukika, kwani kuna umuhimu wa kuweka mifumo mipya ya kuliendeleza Taifa hili.
Umuhimu wa uwepo wa mifumo mipya katika jamii, yetu umedhihirika wazi kwa yaliyotokea katika uchaguzi uluiofanyika mwaka jana.

Ni jambo lililo dhahiri kwamba wananchi wanauhitaji wa mifumo mipya kwani wanaona iliyopo haikidhi kiu yao.

Kulingana na mahitaji haya, kada pekee yenye nafasi ya kuhakikisha hilo linafanyika ni vijana, si kila kijana tu, bali wale wenye nia ya dhati kabisa kuona Tifa letu likiendelea kusimama miaka lukuki ijayo.

Wito huu ni kwa vijana wazalendo, kutumia muda wao kuona katiba mpya yenye manufaa kwa wote inapatikana kwa kushiriki kila hatua.

Litakua kosa kubwa sana kama vijana wakikaa pembeni, na kuacha mustakabali wa maisha yao ya sasa na baadae wakiwa kama wazee ukibaki mikononi mwa wengine.

Wazalendo popote mlipo, tushirkiane kuhakikisha katiba mpya inapatikana, yenye kuweka mifumo itakayoloweka Taifa mahali salama kwa kipindi kirefu baadae.

Heri ya mwaka mpya 2016.
 
Tatizo ni pale issue ya Katiba inapogeuzwa uwanja wa vita vya kisiasa ....Tusiache wanasiasa wajifanye wao ndio wazalendo kuliko wenzao wa Makundi mengine ...
 
Mchakato wa katiba uliharibiwa na wanasiasa wote kwa ujumla
 
Back
Top Bottom