Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Mjadala uliotawala wiki hii inayoisha (naamini utaendelea hadi wiki ijayo) ni kuhusu elimu bure kwa shule za msingi na sekondari za serikali. Wadau wengi wakiwemo walimu walio eneo la tukio wamejaribu kutoa maoni yao na wengi wameonyesha wasiwasi wa kutofanikiwa kwa elimu bure hasa ukizingatia serikali imetoa fidia ya ada tu na kutoa maelekezo ya namna gani pesa hizo zitumike bila kujali kuwa hapo nyuma shule zilitoza michango ya ziada kama ya ulinzi, karatasi na taaluma ili angalau kuziba pengo lililokuwa likibaki kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa ada ya 20,000 kwa mwaka peke yake isingetosha kuendesha shule na walioumia zaidi (na hapa wataendelea kuumia) ni wakuu wa shule wenye idadi ndogo ya wanafunzi kwani watapata mgao kidogo lakini kuna gharama watalazimika kulipia ambazo haziangalii idadi ya wanafunzi mfano ni ulinzi.
Ijumaa wakati Mh. waziri wa Tamisemi akitoa maeleo yake kwenye kipindi cha kipima joto ITV alionekana sana kujiaminisha kwamba hela walizopeleka zinatosha na kukemea mara kwa mara kuwa kusiwe na michango yoyote inayohusisha kuchangisha watoto......yaani tageti kuu, ni mzazi asisumbuliwe kwa lolote kuhusu gharama za mwanafunzi kwani hata vitambulisho vyao imeelekezwa watengenezewe kutokana na hela hiyo.
Baada ya kufuatilia mjadala ule, nilipata maswali kadhaa hasa baada ya kujiridhisha kuwa pesa hiyo iliyogawanywa kwa baadhi ya shule haitoshi hasa ukizingatia kuna shule zimepata hadi mgao wa Tsh.250,000/ ambayo huenda atalipwa mlinzi tu na shule kubaki bila hela na hiyo ni kila mwezi na kila mwanafunzi wa bweni amepangiwa TSH.1,500/- (elfu moja na mia tano kwa siku) ya chakula kuanzia asubuhi chai hadi mlo wa jioni na humo humo uwalipe na wapishi kwa sababu hakuna fungu lingine.
Shule nyingi za serikali zina hali kama hii:

- Walimu wengi wanaidai serikali
- miundombinu ya shule nyingi ni mibovu
- shule nyingi hazina ofisi wala maabara
- nidhamu za wanafunzi ziko chini sana sababu hakuna mwalimu anajishughulisha saaana na mtoto
- walimu wengi wamekata tamaa kwani wengi walishajiaminia kuwa serikali inadharau kada yao na hadi jamii nzima inawadharau
- kila siku na kila mwaka kilio cha walimu ni mishahara isiyoendana na hali halisi ya maisha ya sasa wala ugumu wa kazi yao n.k