Kati ya Ronaldinho,Messi na Pele.Yupi ni Fundi wa kuchezea Mpira na Kunyanyasa Wachezaji wa Timu Pinzani?

endesha

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,109
1,452
Kwakweli Tangu mpira ulipoanza kuchezwa ,Imejipatia Mashabiki kila Pembe Ya Dunia.Na Burudani hasa kwa wale Mashabiki wa Mpira wenyewe.

Lakini Burudani huongezeka pale kunapotokea Wanaume ambao hulazimisha Mpira kutii kile wanachokitaka wao.

Swali ni moja tu kati ya hao ni yupi zaidi wa Kuchezea mpira,Kupiga chenga za Maudhi na Manjonjo mengine yanayoongeza Burudani ndani ya Uwanja?

Mimi si Mhenga,Lakini nimeangalia Clips za Maradona akaniacha Mdomo wazi
 
Wote uliowataja bado hawajamfikia fundi wa mpira, Manuel Francisco dos Santos maarufu kama " Garrincha " au Furaha ya Watu.

Alijaaliwa kipaji cha hali ya juu sana livha ya mguu wake mmoja kuwa mfupi na kujikunja ( tege ) anatajwa kama mkokotaji mahiri wa mpira kuwahi kutokea Ulimwenguni sahau kuhusu upigaji wa chenga za maudhi kwa wapinzani.

Ndiye staa aliyeipa Brazil taji la Kombe la Dunia la mwaka 1962 lililofanyika pale kwa Wahuni na watukutu nchini Chile.
Aliibeba Brazil kwenye makwapa yake mara baada ya kuumia kwa Pele kwenye mechi ya pili tu hivyo Garrincha akavaa vyema viatu vya Pele. Na ndio aliyekuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.
Sema kutokana na ulevi uliopindukia wengi hawakumpa heshima yake na haishangazi alipofariki mapema kutokana na ulevi.
Ni kama stori ya George Best tu.

Hivyo unapolinganisha hao jamaa zako tafadhali naomba umkumbuke na Garrincha katika orodha yako!
 
Nakubaliana na wewe. Kwa tuliocheza soka na kubahatika kuwaona hawa wote hakuna mwenye ujuzi wa kuchezea mpira kama Gaucho. Ndiyo maana wenye imani kidogo waliamini anatumia "super natural power". Haukuwa uwezo wa kawaida. Baadhi ya wachezaji wenzake waliamini hivyo pia na hata kuogopa kumkaba. Lakini Je, Garincha wa Brazil wa enzi hizo hizo za Pele unamweka wapi?
 
Pele alikuwa hajui kuchezea mpira yeye kufunga tu
Mesii anakimbia anadribble anafunga
Dinho ndio freestyler wa mpira aliyeweza kucheza mpira...yaani anauchezea mpira huku anakucheka na anakufunga
Nilikusudia Kuandika DIEGO MARADONA na si PELE
 
Binafisi Gaucho alikuwa bora ktk angle hiyo ya kuuchezea mpira tena kwa mvuto wa hali ya juu muno. Hao wa akina Pele, Maradona na Garincha...sikuwahi kuwashuhudia....
 
weee la pulga messi wote wakasome hao watapata sifa za u legendary tu but sio kumshinda messi
 
Kumweka Pele na hivyo vifaranga ni kumkosea heshima
Wote wameiga kwa Pele
Ukitaka kuniamini nenda youtube
 
Pele alikuwa hajui kuchezea mpira yeye kufunga tu
Mesii anakimbia anadribble anafunga
Dinho ndio freestyler wa mpira aliyeweza kucheza mpira...yaani anauchezea mpira huku anakucheka na anakufunga
Mbona huyo Dinho hajawahi kuipa Barcelona kombe la mfalme?

MESSI ZAIDI
 
Pele alikuwa hajui kuchezea mpira yeye kufunga tu
Mesii anakimbia anadribble anafunga
Dinho ndio freestyler wa mpira aliyeweza kucheza mpira...yaani anauchezea mpira huku anakucheka na anakufunga
Hv wewe umeanza kushabikia mpira lini vitu wanavifanya Leo wakina mess,dinho, ronaldo wote wawil,zizoou na wengneo Pele alishavifanya miaka hamsin iliyopita ACHA KUMFANANISHA PELE NA TAKATAKA ZINGNE angalia Pele documentary ndio utajua Pele alikuwa nani
 
hao unaowataja wameshakiri kuwa GAUCHO hakuna wa kufanana naye!

kuanzia messi, christiano, pele, maradona,, wote wamenyoosha mikono juu,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom