Kati ya Magufuli na Wapinzani (CHADEMA, Zitto & Co.) nani Dikteta?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Inanishangaza na kuniwia vigumu kila siku nikisikia vilaza wa CHADEMA kama Mbowe, Lisu, Zito na wengineyo wakipiga kelele kwamba Raisi wetu Magufuli ni dikteta, sasa tujiulize kiuhalisia kabisa kwa maana halisi ya neno ,,dikteta" nani kati yao anafiti hapo? Yaani linganisha Mbowe na Raisi Magufuli, linganisha CCM na CHADEMA, linganisha Zito na Raisi Magufuli halafu niambie ni nani dikteta?

Tukianza na Zito hicho Chama cha ACT ni mali yake binafsi na yeye ndiyo alfa na Omega wa ACT na yeye ndiyo muamuzi wa kila kitu sasa kama huu siyo udikteta basi nipeni maana yake!

Tukija kwa CHADEMA Mbowe, Chama hata kisichofanya uchaguzi wa kuchagua Mwenyekiti wake, Chama ambacho mwenye chama Mtei amempa mtoto wake Mbowe Uongozi wa Chama, hii ina tofauti gani na Museveni aliyemfanya mke wake Waziri na mtoto wake mmoja kati ya wakuu wa Jeshi la Uganda?

Tukija CCM kila mtu anajua lini kuna uchaguzi wa Chama, Mwenyekiti wa Chama hana ndugu wala mtoto aliyempa uongozi wa Chama, Mgombea wa Uraisi kupitia CCM utaratibu ulifwata na wagombea walishindanishwa kinyume na chadema ambapo fisadi Lowasa alipewa nafasi ya kugombea masaa mawili tangu alipojiunga na Chama hii imetokea wapi kwingine Duniani? hivi kwenye demokrasia ya kweli hili linawezekana vipi?
Yaani mtu ajiunge na Chama kwa mara ya kwanza halafu ndani ya masaa mawili awa bypass wote waliokuwepo kwenye chama tangu siku 0 Chama kinaanzishwa na kupewa nafasi ya kugombea uraisi, hii ni demokrasia ya wapi?
Fisadi Lowasa amepewa nafasi ya kugombea Uraisi CHADEMA wkt hajui hata kitabu cha Katiba ya CHADEMA kina rangi gani achilia mbali hata kujua tu Historia ya CHADEMA, sasa hii ni demokrasia? Ni wapi Dunia hii hili limeshawahi kutokea?
Hili CCM haliwezekani mtu huwezi kutoka ulikotoka hata siyo Mwanachama eti upewe naafsi ya kugombea uongozi ...

Kesho Mbowe akiamua anamfukuza Tundu Lisu na hakuna wa kumfanya Mbowe kitu kama vile alivyomfukuza Slaa ...
 
Nadhani watanzania tulio wengi tunashabikia siasa ukwel hatuutaki!, magu cyo dicteta!

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani watanzania tulio wengi tunashabikia siasa ukwel hatuutaki!, magu cyo dicteta!

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Ni mapema sana kusema kama mh rais ni dikteta au sio tusihukumu kwa hisia na wala tusisifie kwa hisia.
 
Kabla ya kujibu hoja zako inabidi tujiulize kwanza katiba ya chadema inasemaje kuhusu cheo cha mwenyekiti.

Pia tujiulize uteuzi wa Mh. Lowasa kama mgombea wa urais kupitia Chadema kwa uchaguzi uliopita, uteuzi wake ulikua huru na wa uwazi.

Je Mh. Lowasa alipitishwa kwa mtindo wa aina gani kati ya kura ya siri au kura ya wazi.

Tujiulize ni mambo gani yaliyosababisha Mh. Zitto Kabwe kua na utofauti na uongozi wa Chadema mpaka ikapelekea yeye kujivua uanachama na kujiunga na Act.

Je ni kweli Zitto yeye ndio kila kitu kwenye muenendo wa shughuli zote za ACT wazalendo.

Tukishapata majibu ya maswali hayo inabidi tujue na tabia au sifa zinazothibitisha udikteta na vivo hivyo tujue na tabia au sifa zinazothibitisha demokrasia tukishajua na hayo ndio tuoanishe na uongozi wa Mh rais Magufuli ni wa aina gani kati ya hizo mbili tusije tukawa tunakukumu bila ya kua na uthibitisho wa kile tunachohukumu.


#fikrahuru
#mjamaawakweli
 
hacha matusi, husijitoe ufahamu mnapo ambiwa ukweli. vilaza kweli eti mnalalama demokrasia inakandamizwa, ndani ya UKAWA kuna democrasia????!!!!!

Sijaelewa hasa nia ya hoja yenu....ni kulinganisha kiwango cha udikteta au kukanusha udikteta wa rais?

Mtu mjinga hupenda ulinganifu pale tu anapobaini udhaifu hata upande wa mkosoaji lkn kama hakuna udhaifu huwa hana la kusema. CDM, ACT na mengineyo ni taasisi za hiyari, bila shaka kama yupo ambaye inamkera basi atahamia chama kingine. Taifa la Tanzania ni mali ya Watanzania wote, je Mtanzania akikerekwa na udikteta wa rais ahamie wapi?

Nimekuwekeeni ulinganifu si kukataa udikteta au kuukubali kuwa upo kwa huyu na kwa huyu haupo, bali kuwaweka katika mazingira ya kuwa fair mnapojadili mambo. Ukiamka leo ukamtoa mkeo nje uwanjani ukaanza kumkamua maziwa lazima tutakukemea. Lakini utetezi wako ukiwa 'mbona wewe unamkamua ng'ombe wako hadharani' basi wewe ni taahira wa akili.

Acha sio hacha.
 
Akili yako ndogo sana. Uongozi wa chama na wa serikali huwezi kuufananisha hata kidogo. Mbowe au Zitto ni viongozi wa vyama ambao uanachama wake ni suala la hiari. Mtu akiona CHADEMA au ACT kuna udikteta anahama humo na kwenda kwingine hata huko CCM.

Lakini hivi Magufuli akiwa dikteta utahamia Kenya? Au utafanya mchakato aondoke madarakani na ikibidi aadhibiwe? Ni ujinga kama utakuta mtu analalamika kuwa chama chake kina udikteta! si aondoke.
Hata Nyerere aliwahi kusema CCM sio mama yangu, jee uliwahi kumsikia anasema Tanzania sio mama yangu? Nchi ni lazima ipiganiwe maana huna nyingine na upuuzi katika uongozi wake hauvumiliki
 
Mkuu umeleta thread mujarabu kabisa, hawa ufipa wameshikwa pabaya na uncle ngosha , wananchi tumewastukia hatuwaamin tena, ajenda ufisad kwapan
 
Akili yako ndogo sana. Uongozi wa chama na wa serikali huwezi kuufananisha hata kidogo.
Mbowe au Zitto ni viongozi wa vyama ambao uanachama wake ni suala la hiari. Mtu akiona Chadema au ACT kuna udikteta anahama humo na kwenda kwingine hata huko ccm.
Lakini hivi Magufuli akiwa dikteta utahamia Kenya? Au utafanya mchakato aondoke madarakani na ikibidi aadhibiwe?
Ni ujinga kama utakuta mtu analalamika kuwa chama chake kina udikteta! si aondoke.
Hata Nyerere aliwahi kusema ccm sio mama yangu, jee uliwahi kumsikia anasema Tanzania sio mama yangu? Nchi ni lazima ipiganiwe maana huna nyingine na upuuzi katika uongozi wake hauvumiliki
Mbowe ana mwaka wa 12 akiwa kiongozi mkuu wa CHADEMA, hakuna mwenyekiti wa CCM aliyewahi kuka kwenye uongozi zaidi ya muda unaokubalika kikatiba. Hakuna suala la mtu kuwa na influence ya ajabu ndani ya CCM lakini mambo haya CHADEMA yapo na yameshalalamikiwa sana. Issue ya mababy kwanini iliwaudhi wabunge wanawake wa upinzani kama hakukuwa na ukweli ndani yake?.
 
Unajitoa kwa nguvu zote kuandika upuuzi uongo na uzandiki,lini na wapi Mbowe alimfukuza Dr,Slaa.mwenyekiti wa CHADEMA alie muachia Mbowe chama ni Bob Makani tena kwa uchaguzi halali hakuna alie zuiwa kuchukua fomu au kugombea,sasa hilo la Mtei kumpa Mbowe chama linatoka wapi?mtabakia hivyo hivyo kupewa fulana,kofia,na buku saba.
 
Tatizo unafikiri kila asiye mwanaccm basi atakuwa Ukawa au Act wazalendo!Hivi mwananchi wa kawaida unampaje explanation ya namna hii?Hapa iangaliwe serikali ili kujibu kiu ya kila mtanzania,serikali ijieleze kwa kushutumiwa huku na sio kuelekeza vidole kwa wapinzani wao!
 
Mbowe ana mwaka wa 12 akiwa kiongozi mkuu wa CHADEMA, hakuna mwenyekiti wa CCM aliyewahi kuka kwenye uongozi zaidi ya muda unaokubalika kikatiba. Hakuna suala la mtu kuwa na influence ya ajabu ndani ya CCM lakini mambo haya CHADEMA yapo na yameshalalamikiwa sana. Issue ya mababy kwanini iliwaudhi wabunge wanawake wa upinzani kama hakukuwa na ukweli ndani yake?.
Kumbe nawe waweza kuwa bwana mdogo hujui mambo. CCM ndio TANU na TANU ndio CCM ndio maana Sera majengo, viongozi na rasilimali vimerithiwa na ccm.
Nyerere alikuwa Rais wa TANU (CCM) tokea 1954-1977 ambayo ni miaka 23 upo hapo? Pia Mwenyekiti wa ccm miaka 12 sasa mbona unadanganya?
 
Kumbe nawe waweza kuwa bwana mdogo hujui mambo. CCM ndio TANU na TANU ndio CCM ndio maana Sera majengo, viongozi na rasilimali vimerithiwa na ccm.
Nyerere alikuwa Rais wa TANU (CCM) tokea 1954-1977 ambayo ni miaka 23 upo hapo? Pia Mwenyekiti wa ccm miaka 12 sasa mbona unadanganya?

Utaratibu wa miaka 10 ulikuja baada ya Nyerere kung'atuka. Na ni mwenyekiti gani baada ya Nyerere ambaye alipitiliza muda wake aliopangiwa?.

Kwa hiyo Mbowe ndio Nyerere wenu?. Akishafikisha miaka zaidi ya 20 kwenye cheo alichonacho ndipo mtaanza kuwapa muda maalum wenyeviti wenu?.

Hiyo CDM naiona imekaa kama SACCOS fulani hivi ambayo ni maalum kwa wajanja wachache.
 
Mbowe ana mwaka wa 12 akiwa kiongozi mkuu wa CHADEMA, hakuna mwenyekiti wa CCM aliyewahi kuka kwenye uongozi zaidi ya muda unaokubalika kikatiba. Hakuna suala la mtu kuwa na influence ya ajabu ndani ya CCM lakini mambo haya CHADEMA yapo na yameshalalamikiwa sana. Issue ya mababy kwanini iliwaudhi wabunge wanawake wa upinzani kama hakukuwa na ukweli ndani yake?.
Kuhusu kuja juu wabunge kuhusu mababy ilikuwa lazima kwani wametukanwa.
Mbona viongozi wa uvccm walipoambiwa kuwa safari zao za Mombasa zinajulikana kuwa wanaenda kufanywa nini walikuja juu? Unataka kusema kwa kuja kwao juu ile habari kuwa ni mashoga ni kweli?
 
Wako wawili kati yao hamna mtu kwahyo inamaanisha hamna dikteta kati yao
 
Utaratibu wa miaka 10 ulikuja baada ya Nyerere kung'atuka. Na ni mwenyekiti gani baada ya Nyerere ambaye alipitiliza muda wake aliopangiwa?. Kwa hiyo Mbowe ndio Nyerere wenu?. Akishafikisha miaka zaidi ya 20 kwenye cheo alichonacho ndipo mtaanza kuwapa muda maalum wenyeviti wenu?.
Hiyo CDM naiona imekaa kama SACCOS fulani hivi ambayo ni maalum kwa wajanja wachache.
Kwa hiyo Chadema wanatumia katiba ya ccm kuhusu mika 10?
Hivi unajua kazi ya msajili wa vyama? Mkifanya lolote tofauti na katiba anatengua maamuzi
 
Back
Top Bottom