Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ngurumo ya Kitheolojia Katika Moyo wa Roma
Vatican City – Kanisa Katoliki, ambalo limekuwa nguzo ya mafundisho ya miaka elfu mbili, linapitia mojawapo ya enzi zake za utata mkuu, hasa kuhusu masuala ya jinsia na utu wa binadamu.
Kutoka kwa marufuku kali ya vitendo vya ushoga katika Maandiko Matakatifu hadi Azimio la hivi karibuni la Dignitas Infinita (Utu Usio na Kikomo) la Aprili 8, 2024, kunaonekana kuibuka kwa mtikisiko wa kimafundisho unaowaacha waumini na makasisi wengi wakiwa njia panda.
Je, Kanisa linafuata Maandiko Matakatifu au linatengeneza theolojia mpya ya huruma wote?
Swali hili limeibuliwa kufuatia mfululizo wa matukio na nyaraka kutoka kwa Dikasteri ya Mafundisho ya Imani (DDF), inayoongozwa na Kardinali mkuu wa Argentina, Víctor Manuel Fernández. Licha ya Dignitas Infinita kulaani ubaguzi dhidi ya mashoga, wengi wanaona nyaraka za hivi karibuni – hasa uamuzi wa Oktoba 2023 kuruhusu watu waliobadili jinsia (transgender) na mashoga wanaoishi pamoja kuwa mashahidi wa ndoa na wazazi wa ubatizo, na Waraka wa Fiducia Supplicans (Desemba 2023) ulioidhinisha baraka zisizo za kiliturujia kwa wapenzi wa jinsia moja – kama kupingana moja kwa moja na Msimamo wa miaka ya nyuma wa Kanisa, na hata Maandiko Matakatifu yaliyotajwa.
Utata huu unazua mjadala mzito, si tu katika mitaa ya Vatican bali pia kwenye jumuiya mbalimbali haswa barani Afrika na kwingineko duniani. Wengi wanajiuliza: Ni nini hasa kimebadilika kati ya Marufuku ya 2021 ya DDF na roho ya "utu usio na kikomo" ya 2024?
Hoja ya msingi ya wakosoaji, kama inavyoonekana katika marejeo ya Biblia yaliyotolewa, inategemea maandiko yaliyofafanuliwa ambayo yanayokataza vitendo vya ushoga kwa uwazi:
Mwanzo 19:1-13 (&Kisa cha Sodoma na Gomora*).
Vivyo hivyo Mambo ya Walawi 18:22 na 20:13: Hizi ziko wazi: "Usimlale mwanamume kama ulalavyo mwanamke; ni chukizo." Ya pili inaongeza hukumu ya "wauawe kabisa."
Warumi 1:26-27: &Mtume Paulo* anaelezea "shauku chafu" na "kubadilishana mahusiano ya asili na yale yasiyo ya asili" (kama anavyosema kuhusu wanawake na wanaume) kama matokeo ya kumkataa Mungu.
1 Wakorintho 6:9-10 na 1 Timotheo 1:9-10: humo tunaoneshwa kuwa "wanaofanya ushoga" kama wasiorithi ufalme wa Mungu.
Mtazamo wa Awali wa Kanisa (Kama Unavyoonekana na Wakosoaji)
Msimamo wa Kanisa la Katoliki kimila umesisitiza tofauti kati ya mtu mwenye mvuto wa jinsia moja (anapaswa kupokelewa kwa heshima) na kitendo cha ushoga (kinachukuliwa kuwa ni "kwa asili hakina mpangilio wa kimahusiano" na ni dhambi). Huu ndio msingi na roho ya hati za zamani kama vile Homosexualitatis problema (1986).
Hata Msimamo kama ule wa Marehemu Askofu Mkuu Amato mnamo Aprili 2007, alipokemea ndoa za jinsia moja na kutoa hoja kuwa ni "maovu yanayoonekana kama maendeleo," tunapaswa kuishi na theolojia ambayo inalinda mfumo wa ndoa takatifu kati ya mwanamume na mwanamke pekee, kulingana na mafundisho ya Donum vitae (1987) kuhusu heshima ya uzazi. Marehemu Askofu Mkuu Amato hakuwahi kuwa na moja kwenye mbili linapokuja suala la kiroho.
Utata upo wapi? DDF inapingana na Nini Haswa?
Wakosoaji wanadai kuwa DDF, chini ya uongozi wa Kardinali Fernández anayejulikana sana kama mshauri wa karibu wa Papa Francis na Papa Leo, imepoteza dira na kwenda mbali na msimamo huu wa kimila.
Responsum (Machi 2021) dhidi ya Fiducia Supplicans (Desemba 2023):
Mnamo 2021, DDF ilisema wazi: "Kanisa halina, na haliwezi kuwa na, uwezo wa kubariki miungano ya watu wa jinsia moja." Lakini mwaka 2023, katika waraka wa Fiducia Supplicans ikaruhusu baraka za watu binafsi katika muungano ya namna hiyo, kwa masharti la kwamba baraka hiyo isifanane na ibada ya ndoa takatifu.
Hii ndiyo hatua iliyozua hasira kubwa kimataifa. Wakosoaji wanaona huu ni mabadiliko ya kimafundisho yasiyo ya moja kwa moja, huku Vatican ikisisitiza ni "hizo ni baraka za kichungaji" na si "takwa wala idhini ya kitheolojia ya muungano."
Dignitas Infinita (Aprili 2024):
Ingawa hati hii inalaani vikali nadharia ya jinsia (gender theory) na kubadili jinsia kwa upasuaji kama ukiukwaji wa utu wa asili, Lakini pia inalaani ubaguzi wote dhidi ya ushoga na mashoga. Ni hati ya utu wa binadamu, inayojumuisha umaskini, vita, na ukatili wa kidigitali. Utata kwa wakosoaji uko katika ukweli kwamba Vatican inakataa dhana ya jinsia ya kuchagua huku ikikubali kubariki miungano ya watu wanaoshikilia utambulisho wa jinsia moja, na kuruhusu watoto wa wapenzi wa jinsia moja kubatizwa.
"Swali la msingi sio baraka; swali ni kuegemeza vitendo hivi karibu na huruma huku tukipuuza ushahidi wa wazi wa Maandiko Matakatifu kuhusu dhambi," anasema mwandishi wa theolojia Padre James Mwangi (Jina limebadilishwa kwa sababu za kiusalama).
Mpasuko na Mgawanyiko wa Kimataifa:
Msukumo huu wa kichungaji kutoka kwa aliyekuwa Papa Francis na Kardinali Fernández umegawanya vyeo vya Kanisa (Hierarchy) katika pande mbili kuu: Utii na Upinzani.
A. Papa na Viongozi Wakuu (Pope, Cardinals, Archbishops Wanaoungwa Mkono)
Papa Francis alipenda kujikita zaidi katika Theolojia ya Huruma, akisisitiza kwamba Kanisa lazima liwe "uwanja w amani na upendo" na likaribishe watu wote, hasa wale walio pembeni mwa jamii, bila kughairi mafundisho ya msingi ya Kanisa. Yeye na Kardinali Fernández waliona Dignitas Infinita kama mkakati wa kuonesha kwamba msimamo wa Kanisa wa kutokubali matendo ya ushoga hausababishi ubaguzi au unyanyasaji wa mtu aidha akiwa ni shoga au sio shoga.
Kardinali Fernández: Ameeleza (kama ilivyotangazwa kwenye vyombo vya habari) kuwa lengo ni kumkomboa Mungu kutoka kwenye mfumo wa kiadili uliojaa "ubaguzi na vitambulisho," ambao ulikuwa na nia ya "kuainisha watu." Anasisitiza kuwa Utu wa Binadamu (Dignity) haupunguzwi na dhambi au hali ya maisha.
B. Upinzani Mkuu (Maaskofu na Makardinali Wachache)
Upinzani mkali zaidi umekuja kutoka kwa Maaskofu wa bara la Afrika (kama vile Ghana, Malawi, Zambia, Tanzania), ambao walikataa kwa pamoja Fiducia Supplicans (Waraka wa baraka) kwa sababu za kitamaduni, kimaandiko, na kichungaji (wakihofia kuwa itachanganya waumini wao).
Askofu Mkuu Mmoja wa Afrika: Alisema: "Hatuwezi kubariki kile ambacho Mungu amekiharamisha. Baraka hii ingeweza kufundisha waumini wetu kwamba dhambi inakubalika." Cardinal Fridolin Ambongo Besungu (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Cardinal Robert Sarah (Guinea), Cardinal Gerhard Ludwig Müller (Ujerumani) ambaye huyu alishinikiza kwamba mapaji ya baraka kwa watu wenye mahusiano ya jinsia moja yanakiuka mafundisho ya Kanisa Katoliki, na huku pia akikosoa vikali bunge la maaskofu wa Ujerumani (German Synodal Way) kwa kuunga baraka za mahusiano ya jinsia moja.
Makardinali Wachache Wazee (Wanaojulikana kama 'Dubia Cardinals'): Wameonyesha wasiwasi wao juu ya hatua hizi, wakisisitiza kwamba Mapokeo (Tradition) lazima yasipuuzwe kwa ajili ya usasa.
Mfano ni Cardinal Raymond Leo Burke (Marekani), Cardinal Juan Luis Cipriani Thorne (Peru), Cardinal Carlo Caffarra (marehemu) ambaye alikuwa ni mkosoaji mkuu wa mafundisho yanayotaka kubadilisha msimamo wa Kanisa juu ya ndoa na mahusiano ya jinsia moja.
C. Makasisi, Mashemasi na Waumini (The Laity)
Makasisi na Mapadre (Priests and Deacons): Wengi wamejikuta katika hali ngumu. Wameapa utii kwa Papa lakini wanakabiliwa na ukweli wa Maandiko Matakatifu na waumini walio na hasira au waliochanganyikiwa katika parokia zako.
Mfano, Kardinali Robert McElroy wa diosisi ya San Diego amekataa na kugoma kabsa kutoa baraka kwa wanandoa mashoga, huku pia akizuia ufasiri wa hati ya Fiducia Supplicans. Vivyo hivyo, Archbishop Philip Anyolo wa Nairobi (Kenya) alitoa maelekezo kuwa mapadri na walei wasifuate chochote kuhusu Fiducia Supplicans bali wafuate miongozo sahihi yenye kuleta ustawi, Archbishop Philip Anyolo aliungana bega kwa bega na ambacho kilizungumzwa na Bishop Flavian Matindi Kassala.
Mvutano huu katika Kanisa Katoliki unahusu zaidi jinsi ya kutafsiri Utu wa Mwanadamu katika theolojia. Dignitas Infinita haikubadili mafundisho ya Kanisa kuhusu tendo la ushoga (bado ni dhambi na haina maelezo ya kupindisha ili ujumbe uonekane unavutia), bali imesisitiza kuwa utu wa Mtu (The Person) hautoweki hata kwa dhambi, na ubaguzi ni ukiukwaji mkubwa wa utu huo (kama umaskini au vita).
Kwa Kardinali Fernández na aliyekuwa Papa Francis, kumpa mtu baraka haimaanishi kuidhinisha au kukubaliana na dhambi zake, bali ni kumkaribisha kwenye njia ya uongofu na kumwonyesha upendo usio na kikomo wa Mungu.
Kwa wakosoaji wa Biblia, hatua hii inaweka historia mpya ya kichungaji ambayo inafifisha mstari kati ya dhambi na neema, na hatimaye, inapingana na mapokeo ya kitheolojia na kibiblia yaliyowekwa na mababu wa Kanisa. Kuanzia Papa wa kwanza, Mtakatifu Petro, Papa Leo Mashuhuri, Papa Gregory Mashuhuri, na mapapa wengine Zaidi ya kumi.
Swali kuu linabaki ni; Je tunapaswa kubadilisha tafsiri za Maandiko na mafundisho ya kanisa katoliki ili kuwavutia wengi ama kuwabadilisha wengi?
ANGALIZO: Mimi ni Mkatoliki na sina nia mbaya ya kuchafua kanisa letu kwa namna yoyote na haya ni mawazo yangu tu!