Kata ya Bugarama Kahama kuchukuliwa rasimi na UKAWA

Kata ya Bugarama Kahama kuchukuliwa rasimi na UKAWA

kambagasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
2,271
Reaction score
1,809
Habari zenu wadau, Katika mkoa Shinyanga Kahama jirani kabisa na Kakola kuna kata ya Bugarama ambayo kwa kila dali awamu hii lazima ichukuliwe na UKAWA. Picha lenyewe liko hivi; Katika uchaguzi uliopita wananchi waliionyesha CCM kuwa wao si mburura tena baada ya kijiji cha Ilogi kutetewa na CHADEMA huku Bugarama CCM na CHADEMA kugawana vitongoji nusu kwa nusu kwa mara ya kwanza tangu vyama vingi.
WATIA NIA WA CCM
Watia nia wa CCM ni kichekesho kwani wengi ni watuhumiwa wa kuifilisi SACCOS kubwa ya IBUKA kabla hawajaitelekeza na kukimbilia kuwania udiwani huku wakielekeza mashambulizi kwa diwani anayemaliza muda wake na huku akiwa ametangaza nia tena huku akiugwa mkono na kijiji anachotokea tu (BUYANGE). Kichekesho kingine ni watia nia kutoka vijiji vya Bugarama,Igwamanoni na Ilogi ambao kama kuna watu wanawaunga mkono basi ni waganga wa jadi na wachawi huku kundi kubwa la vijana ambao wamejiandikisha kwa wingi wengine wakijiandikisha wakitokea Kakola ambayo ni ngome ya UKAWA wakimpigia upatu bwana Izengo wa CHADEMA kama chaguo lao. Kuna kijana mmoja wa CCM ambaye sitamtaja alikuwa ametangaza kugombea kwa kupitia CCM nasikia ameandika barua ya kujitoa katika ulingo kwa kutishiwa kulogwa na hao wazee wanaotaka udiwani kwa tiketi ya CCM. Msiulize nimezipata wapi kwani nilikuwa huko kabla sijarudi kwangu Bariadi.
 
....ukiwa ccm utakuwa mchawi tu, hongera ukawa pasueni vichws magamba mpaka yapagawe...
 
Hii ni kweli kabisa.Kile kitu cha pale sokoni kwa asilimia kubwa kimeandikisha watu wengi kutokana Kijiji jirani cha KAKOLA ambako ndiko kwenye ngome ya UKAWA kwa wilaya mpya ya msalala.
Kwa aslimia 98.9% nakubaliana na wewe mleta Uzi.Ccm imeshaagwa rasmi kwenye KATA ya BUGALAMA.
 
Hii ni kweli kabisa.Kile kitu cha pale sokoni kwa asilimia kubwa kimeandikisha watu wengi kutokana Kijiji jirani cha KAKOLA ambako ndiko kwenye ngome ya UKAWA kwa wilaya mpya ya msalala.
Kwa aslimia 98.9% nakubaliana na wewe mleta Uzi.Ccm imeshaagwa rasmi kwenye KATA ya BUGALAMA.

Mkuu mie nilicheki kile kituo cha ofisi ya mtendaji watu waliojiandikisha juzi na jana asilimia kubwa si wakazi wa Bugarama viongozi wa CCM sijui kwa nini hawajashitukia hili:what:
 
Nimepiga simu na kuhakikishiwa kabisa ni kweli yule kijana amewaachia wazee na kuna tetesi kuwa amesema endapo Lowassa (shabiki wa Lowassa) atakatwa yuko tayari kujiunga CHADEMA na kuwapeleka mpera mpera hao wazee wakisaidiana na Izengo ambaye wamesoma nae Mwanza na kuajiriwa pamoja mgodini kabla hajaacha kazi na baadaye akaamua kujiajiri.
 
Usipumbazwe na uwingi wa watu kutoka eneo moja kwenda kujiandikisha sehemu nyingine. Tatizo ni upungufu wa mashine za BVR ukilinganisha na idadi ya watu kwenye baadhi ya maeneo, maeneo waliyotoka watu wanakesha kusubiri kuandikishwa na wengine wanafanya biashara kati ya shilingi 5000 mpaka 20000 kuuza nafasi kwenye foleni. Suluhisho pekee la kuweza pata hicho kitambulisho cha mpiga kura ni kuulizia maeneo ambayo hamna foleni na kwenda kujiandikisha ili kukwepa kadhia ya foleni na kusukumana. Kwa mantiki hiyo mkuu wanao kuja kujiandikisha huko si kwamba wanataka kuitoa CCM bali kuna sababu nyingine kabisa nawe wape elimu watu wako kuwa mabadiliko hayaletwi na watu wa kuja kwa msimu bali yanaanzia na wakazi husika.
Pia natumai unafahamu maana ya neno ILOGI kwa lugha ya kisukuma na historia ya eneo husika kama ulivyo elezea basi unganishi hizo dots na uelewa wa watu wa eneo hilo ili uwape elimu ya mageuzi ya kifikra na mitazamo.
 
sasa ccm kwauchaguzi huu ngome yao niwapi?

Ndugu mimi si mtabiri kama shekhe Yahaya lakini CCM ilitakiwa watafute mtu anayeuzika kwa makundi yote. Yule aliyejitoa alikuwa anakubalika hata kwa wapinzani lakini ameangilia na kugundua hakuna duka la spea ya moyo😛:sly: Kwa kifupi ngome ya CCM iko kwa waganga wa jadi kama nilivyoelezea hapo juu. Kumbuka hii kata ni moto sana kwani diwani aliyeshinda kihalali aliuwawa kwa mapanga na aliyemuua nayeye akafia Guest House Shinyanga mjini akiwa mkimbizi.
 
Namfahamu marehemu diwani Paul Kisiminza aliuwawa kikatili sana,wananchi wa Buyange wakaandamana kwenda kuchoma nyumba ya diwani aliyetuhumiwa lakini polisi wa Ilogi wakawatawanya ikabaki vita ya "unga mweusi" hadi mwishoni mwa mwaka Jana yule mtuhumiwa akakutwa amekufa peke yake Shinyanga kwenye nyumba ya wageni.
 
Back
Top Bottom