Kwa kipindi kirefu meya wa manispaa ya bukoba kule kagera amekuwa katika msuguano wa kisiasa na mbunge wa jimbo hilo Balozi Kagasheki.kila mtu anajua kuwa mgogoro huo uliundiwa tume na haijatoa majibu.lakini kabla tume haijatoa majibu tayari serikali imemuahmisha mkurugenzi wa hapo.Sasa huko mimi siko.
Taarifa nilizopata kutoka kule kagera(na mtoto wa jamaa yangu ni mhanga) ni kuwa Meya huyo anafanya mchezo wa ajabu sana kwa shule zake anazomiliki.(Aman primay,peace sekondar nk).
alichokuwa akifanya tangu nyuma ni kuwatapeli wanafunzi wanaokuwa wakilamaliza kidato cha nne amabo anaona wanaweza kupata division 0 au 1V.anachofanya ni kuwahamishia katika shule nyingine bila wazazi wao watoto kujua:Anachofanya ni kuongea na baadhi ya shule ikiwemo Sekondari ya BERNARD iliyoko wilayani karagwe.(yahani mwanafunzi anasoma AMAN lakini number yake ya mtihani iko Bernard au kwingineko.
sasa katika mkutno wa wazazi uliofanyika hivi karibuni shuleni hapo wameelezwa na timu ya uchunguzi iliyoundwa na mkoa wa kagera kuwa wanafunzi zaidi ya 102 hawana usajiri shuleni hapo licha ya kusoma hapo na kuwaomba wazazi wenye watoto ama kuondoa watoto wao au kuongea na mmiliki huyo (aman) ili wajue la kufanya.
katika mwaka 2011:TATIZO HILI LILIJITOKEZA KATIKA SHULE YAKE SOMA HAPA
Sekondari ya Meya wa Bukoba inavyowatapeli wanafunzi
binafsi jamaa yangu mtoto wake yumo kwenye hii list mpya ya waliopelekwa kwingine licha kulipa karo kwa huyo meya.
nitaingiza hapa barua kadhaa na documents mbalimbali na maelezo juu ya meya huyo wa CCM anavyotumia nafasi yake kualimu elimu nchini na mengine mengi.
watu wa siasa mkae kando,sionglei siasa hapa tafadhali!
Nitarejea: