Kashangae Feri,mjini hapa!

Micheweni Pemba

JF-Expert Member
Jul 13, 2010
351
179
“Mchina mwanzo shusha…” ni kauli ya tingo wa gari ya abiria maarufu kama dala dala ambayo nilikua nimo ndani nikirapa kuvuta hewa safi na kupata angalau upepo, kijua kinawaka huku ndani tukiwa tumesheheni tingo anaendelea kunadi na kuengeza abiria zaidi badala ya mmoja wa abiria kushuka hapo, kwa mbwembwe za aina yake anaingiza abiria zaidi kwa kauli “songa mama songa, ingia ndani haiijai hii”

Mama akajaribu kuingia ndani ya dala dala na alivyojaaliwa mwili anajifikicha fikicha na kufanikiwa kuingia ndani ya gari huku mmoja wa abiria wa kiume aliye pembeni yake akibaki kulalama tu na kumuambia, “Mama tartibu na mzigo wako!” Vicheko vikatawala humo ndani licha ya adha yote hiyo.

Usafiri wa gari za abiria Zanzibar umekua ni kama hivyo, bora abiria (punda) afe lakini mzigo ufike! Pale nilipokaa nikiwaza mawazo ya kila aina, yote nikakosa jawabu na mojawapo kuu nikijiuliza “Hivi kuna ulazima wowote wa kupakia binadamu ndani ya gari kama hivi?”

Kwa mshangao ulioje mbele kabla ya kituo kinachofuatia naona tunasimamishwa na nguo nyeupe, yangeyange maarufu trafiki, nikajisemea kimoyo moyo, “haya sasa tamaa yote hii ya kupakia watu kinyume na sheria gari imeshakamatwa.”

Trafiki kasogea upande wa kioo cha dereva na moja kwa moja akaambiwa aweke gari pembeni, bwana trafiki akafoka kwa hasira “weka gari pale umezidisha abiria namna hii!” Sijui walicho wakizungumza trafiki na dereva yule, ila mara yule konda wetu mwenye mbwembwe akashuka na kusogea mbele pembeni ya gari, mazungumzo yao yakaendelea kule na ghafla ya kurudi anamwambia dereva “twende, twende SOS wamo, shusha SOS?” Hee!

Nikapata jawabu la ghafla, kumbe hii kupakiwa namna hii kwenye hizi gari za abiria sababu yake ni hii, ikiwa waliopewa jukumu la kuangalia sheria za barabarani zinatekelezwa kumbe wao wenyewe ni utelezi, kweli tutafika? Ikanijia sura ya tukio la kuzama kwa mv spice na kutuulia watu wetu, msiba usiokauka hadi leo wenzetu wale wengine hawakupatikana wala kuonekana tena.

Nikiwa nasubiri kukata barabara na kanzu langu huku natizama upande wa kulia kwangu nahisi kitu kinanisukuma, Subhanallah, geuka kushoto naona gari inanisukuma, dereva anarudi rivesi kwa mbwembwe za Kiunguja, mkono mmoja kaeka kisambusa, si unajua vile wanaupinda na kueka juu ya kioo, wapita njia wanaampigia kelele “wee utaua wewe
…”

Kwa hasira namfuata dereva kumlaumu, “wewe ni dereva gani wewe usietizama nyuma?” namuuliza, haki ya Mungu jibu lake ni hilo la kichwa cha habariya mada yetu hii “Acha kushangaa shangaa, kashangae feri mjini hapa.”

Nikabaki kushangaa z
aidi na kujiuliza suala lisilo jibu, hivi huyu dereva ananiambia nikashangae feri kwa kujiamini kupi baada ya kutaka kuniua, hata samahani hana licha ya yeye kuwa ndie aliekosea! Huko feri kuna nini hata anielekeze nikashangae huko? na anamaanisha nini kuniambia hapa ni mjini?
Aah nikaamua iwe basi tu, ni yale ya sharia kuwekwa mikononi mwa wachache, Zanzibar imerogwa na mganga wake ameshakufa.
ferry.jpg
 
Back
Top Bottom