kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,685
DAR ES SALAAM.
KIPA Juma Kaseja yuko tayari Mkataba wake Yanga SC uvunjwe iwapo klabu hiyo haitatekeleza mambo mawili, moja kuanza kumpa nafasi za kudaka katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kupitia Meneja wake, Abdulfatah Salim, Kaseja ameipa masharti Yanga SC kama inataka kubaki naye immalizie dau lake la usajili Sh. Milioni 20 na pia kuanza kumpa nafasi ya kudaka.
Kwa sasa, kipa huyo namba moja wa zamani wa Tanzania, hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga SC chini ya kocha Mbrazili, Marcio Maximo, tofuti na ilivyokuwa chini ya kocha aliyetangulia, Mholanzi, Hans van der Pluijm alikuwa anadaka kwa zamu na Deo Munishi.
Abdulfatah ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, katika Mkataba wao walioingia na Yanga SC, walikubaliana kukamilishia malipo ya mwisho ya dau la usajili ya (Sh Milioni 20) ifikapo Januari 15, mwaka huu, lakini klabu hiyo hadi sasa haijafanya hivyo.
Amesema wakati wanavumilia hilo, bado mteja wake hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza jambo ambalo ni hatari kwa kipaji cha kipa huyo.
Abdulfatah amesema kwamba wanayaingiza masharti hayo yote kwa maandishi na kuyapeleka kwa uongozi wa Yanga SC uyatekeleze, vinginevyo hatua za kuuvunja mkataba zitafuata.
Source: Meneja wa Juma Kaseja; Abdulfatah Salim.
BIN ZUBEIRY BLOG