Tambi au pasta ni moja ya vyakula ninavyovipenda sana.Ni rahisi kuandaa na kuna namna nyingi sana ya kuziandaa na kuzipika. Kutokana na uandaaji au upishi tambi zinaweza kutumika kama appetizer,kama chakula kikuu na kama dessert.
Mahitaji Tambi paketi moja(Santa Lucia) Sukari ¼ kikombe au kwa ladha upendayo Iliki Kijiko 1 cha chakula au kwa ladha upendayo(mbegu za iliki zilizosagwa) Maji kikombe 1 1/2 au zaidi Maziwa fresh kikombe 1 au tui zito la nazi Mafuta yatokanayo na mimea 1/2 kikombe au zaidi
Njia 1.Chemsha maji,weka kando.Chemsha maziwa,weka kando. 2.Katika sufuri au kikaango weka mafuta,ongeza tambi,kaanga tambi kwa moto mdogo sana adi zibadilike rangi na kua Brauni.
3.Ongeza maji ya moto (kua makini mvuke usikuunguze),ongeza sukari na iliki,changanya,funika vichemke.Ongeza moto uwe wa wastani.
4.Maji yakielekea kwisha ongeza maziwa ya moto,changanya.Acha vichemke uku ukigeuza mara kwa mara ili tambi na maziwa visinate kwenye sufuria. 5.Maziwa yakielekea kukauka,punguza moto,acha adi maziwa yakauke kabisa kisha fanya kama unakaanga tambi ili kuhakikisha zinakauka .Zikiwa tayari tambi zitakua na matone meupe madogomadogo kama zimemwagiwa nazi ya unga.Tayari kwa kula.
JUA:Mafuta ni kiungo muhim kweneye pishi hili,ukiweka mafuta kidogo sana,hutapata matokeo mazuri.Tambi hazitakaangika vizuri mwishoni. Chakula hiki hupendwa sana na watoto,ni vyema kukiloanisha na mchuzi au sosi ili mtoto ale kwa urahisi. Unaweza remba chakula hiki kwa kutengeneza uso wa mdoli,mauwa na michoro mengine kwa kutumia mboga za majani au matunda ili kumvutia mtoto kula.