Noncommited
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,125
- 369
KARATU ITUNUKIWE TUZO MAALUMU YA UJASIRI, UTHUBUTU NA DEMOKRASIA ILIYOTUKUKA TOKA KWA CHADEMA
Chadema Waitangaze Karatu Kama Jimbo La Kiini Cha Mabadiliko Ya Kweli Na Kupewa Zawadi Maalumu
Kumbukumbu zinaonyesha Karatu ni moja ya Majimbo Vinara kwa Demokrasia nchini Tanzania hasa hasa Tanganyika. Toka 1995 Karatu haijawai kuongozwa na chama cha Mapinduzi.
Historia inaonyesha kwa mara ya kwanza ndani ya Mfumo wa Vyama vingi Jimbo la Karatu likaenda Upinzani TENA CHINI YA Chama kidogo sana kwa wakati huo kiitwacho CHADEMA, Kumbuka vyama vikubwa kwa wakati huoo vilikuwa NCCR, UDP NA CUF.
Karatu ikaongowa na Mbunge wa upinzani Dr.Slaa kwa vipindi Vitatu mfululizo 1995-2010 huku CHADEMA ikiiongoza Halmashauri ya Karatu toka mwaka 2000-2015 bila kupoteza hata muhula mmoja. Kwa CHADEMA kushika halmashauri kuliambatana na Ubunifu wa kuwajali wananchi kwa kuwaondolea Kero za Kodi na michango isiyo na Tija kama vile kodi za baiskeli na michango ya mwenge, vitu vote hivyo kufutwa kwake kulianzia Karatu.
Karatu ikakumbwa na Misukosuko miwili mikubwa iliyosomba wabunge wengi wa Upinzani na uuaji wa vyama vya upinzani: Msukosuko wa kwanza ilikuwa kuhimili Mfagio wa Rais mstaafu JK MWAKA 2005 ambapo alifagia wapinzani wengi sana kwa Nyota yake, Msukusuko wa pili mkubwa ni kitendo cha Dr.Slaa kukikacha CHADEMA na kuipaka matope kibao, wengi wa wachambuzi wakajua CHADEMA watalikosa Jimbo hilo mwaka 2015 kwa kuzingatia Dr.Slaa ndiye aliyeijenga CHADEMA kule Karatu na kuweka Ngome yake lakini matokeo yakawa sivyo, tumeshuhudi Lowasa akiiongoza KURA za urais na CHADEMA kushinda Ubunge mpaka Halmashauri. Hakika msemo wa Fuateni Maneno yangu na siyo matendo yangu muda mwingine una mantiki sana-kwa maana kwamba wana Karatu walifuata maneno na Dr.Slaa aliposema CCM ni mbaya lakini hawajafuta matendo ya Dr.Slaa kuikacha CHADEMA na kuinanga.
Lengo Kuu la Hii Thread ni kuwaomba Viongozi wa CHADEMA walilimulike Jimbo hili na kulipa heshima ya Kutosha kwa kuboresha Huduma za Kijamii kupitia pesa za Ruzuku na kufanya HARAMBEE MOJA KUBWA ya kuchangia jimbo la KARATU ili watu wa uko waweze kufaidi matunda yao ya kuichagua CHADEMA kwa kipindi chote hicho maana siamini kwamba CHADEMA walikuwa na wagombea bora sana kushinda CCM kwa vipindi vyote hivyo bali IMANI NA MAPENZI YA DHATI YA WANA KARATU KWA CHADEMA.
Kitendo cha kuwaandalia TUZO MAALUMU na shukrani kwa wana KARATU kitaleta tija sana kwa Majimbo mengine kujifunza na kuwa na ARI ya kuwa kama KARATU kupitia uwakilishi wa CHADEMA.
MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI UKAWA, MUNGU IBARIKI KARATU, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.