Karani: Ongezeko la mshahara(23.3%) litaniwezesha kumjengea baba yangu nyumba na kumnunulia gari. Bulembo asema mishahara haikuongezwa miaka 6

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,458
7,837
Karani katika halmashauri ya Muheza jijini Tanga, Saum Juma amesema ongezeko la mshahara lililotangazwa na Rais Samia Suluhu litawanufaisha kwa vitu vingi ikiwemo kununua viwanja, kujenga nyumba, kusomesha wadogo zao, kuwasaidia baadhi ya ndugu zao matumizi mbalimbali.

Akijitolea mfano yeye, kasema mshahara ukiongezeka ataweza kumjengea baba yake nyumba, kumnunulia gari kutokana na ongezeko hilo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo amesema watumishi wa Wilaya ya Muheza wamemshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa ongezeko la mshahara la 23.3%.

Halima Bulembo amesema yeye kama kiongozi wao watumishi walimfata na kumwambia kwa kuwa rahisi yeye kumfikia Rais, amfikishie salam zao kwani inatambulika watumishi walikuwa hawajaongezewa mishahara kwa miaka sita sasa na mama kawaongezea mwaka wa 7.

Watumishi wamesema wanamuombea Mama Samia kwa Mungu

Your browser is not able to display this video.
 
Mimi nitanunua Ford Ranger 🤗
 
Huyu nae ni mnafiki fulani hvi. Chukulia mshahara wa chini ni laki tano, ongezeko la 23.33% need sh. 116500/=. Sasa kiasi hicho, ili uweze kununua Corolla ya mtumba 8,000,000/= itakuchukua miaka zaidi ya saba. Sembuse nyumba! Hata Kama ni mbavu za mbwa sio chini ya miaka 5. Acheni sifa za kinafiki.

Bro acha unafiki Mungu hapendi hivo. Kama unalipwa say take home yako ni 3,000,000, angalau sawa, hata ukiongezwa 10% ni 300,000.
Lakini kima cha chini ajivunie nin?
 
Huyu nae ni mnafiki fulani hvi. Chukulia mshahara wa chini ni laki tano, ongezeko la 23.33% need sh. 116500/=. Sasa kiasi hicho, ili uweze kununua Corolla ya mtumba 8,000,000/= itakuchukua miaka zaidi ya saba...
Kwanza unaongelea Corolla ipi? Na mtumba unaomaanisha ni used bongo au used from Japan?
 
Okay ni Vema na Haki...

Ila wale majority vipi wasio na bima wala kujua kama jioni watakula hawana ndoto za hata kupanga mpanga mwisho wa mwezi let alone kujengea wazazi wao! Hao hao sio watanzania?

Na siongelei waongezewe au kupewa chochote atleast hata wapate ujira wa kuhakikisha wanapata mkate wao wa kila siku kwa kuweza kufanya ajira yoyote.

Hizi asilimia sijui ngapi wala sio cha kujisifia ni kama mtu amepewa wajibu wa kupanga matumizi ya pesa zenu ni kuamua tu ampe nani na aache nani (hio sio ngumu hata kidogo) Ugumu ni kuhakikisha anatengeneza mbinu za kuzalisha hizo pesa ili kuweza kuwapatia wote ili waendelee kuchangia vizuri.
 
Ongezeko la 23% Limempa Karani uhakika wa Kumjengea Nyumba pamoja na kumnunulia Gari Babake..

Good.
 
Wewe sio mtumishi una ufahamu wowote hiyo pesa unayoizarau anaweza kuikopea na kupata hiyo milioni 8
 
Ongezeko lenyewe ni elfu 60 lakini linaimbwa na hapo kuna kodi juu yake
 
Yeye mwenyewe haimtoshi hata kula lakini kwa vile ni pumbafu atasifia na ukute amelazimishwa kusifia
 
Pia hapo kuna kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…