Kanuna kama kawaida ya wanawake

mtu bati

Senior Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
117
Reaction score
129
Kuna mpenzi wangu tulikuwa pamoja. Anakuwaga na tabia ya kununa nambembeleza anarudi kawaida.

Sasa Jumapili alikuja kwangu akanitunuku vizuri tu. Sema Kuna kitu kidogo nilifanya akakereka. Aliniuliza swali nikamuambia tulishaongea asiulize muda huo akawa kamind kidogo. Tulimaliza akaenda vizuri tu.

Tukachat kuwa kafika lakini nimemkera. Ila kesho yake aligoma kupokea simu, hata text hajibu mpaka now. Kanuna. Sasa nambembelezaga anarudi kawaida. Now naona kanikazia kanuna kweli kweli. Text hajibu kakaa kimya.

Mwanamke wa kununa nuna hivyo mnamfanyaje? Mimi nimeamua kwenda naye mdogo mdogo tu. Hebu semeni nichukue maujuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…