Kanisa: Serikali iache kuigiza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MAADILI kwa watumishi wa umma yameporomoka kutokana na viongozi hao kutomjua Mungu.

Ni kauli ya Christopher Madole, Askofu wa Kanisa la Gospel Ministry Jimbo la Dodoma aliyoitoa jana alipokuwa akihubiri katika kanisa hilo lililopo viwanja vya Reli mjini Dodoma.

Alikuwa akiendesha ibada ya Siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambapo amesema, umefika wakati sasa wa wanasiasa na viongozi mbalimbali serikalini kuwa na hofu ya Mungu na sio kuigiza.

“… namshauri Rais Magufuli (Rais John Magufuli) aongeze wizara moja tu ya maadili ambayo waziri wake asitokane na chama chochote cha siasa.

“Maana tunaona kuna wakati mawaziri wanaonekana kutetea vyama vyao sasa hii wizara ya maadili itakuwa inasimamiwa na kiongozi wa kiroho,”amesema Askofu Madole.

Amesema kwamba, kutokana na kuporomoka kwa maadili, mawaziri na wabunge wamekosa aibu na hata kuwa na maneno ya kashfa ndani ya Bunge.

“Kumekuwepo na maneno ya kashfa hata ndani ya bunge, mfano; mbunge anasema sizungumzi na mbwa bali nazungumza na mwenye mbwa au kusikia mbunge anasema funga milango tupigane,” amesema.

Askofu Madole amesema kuwa, yote hayo ni dalili ya watu kukosa hekima na busara na zaidi ni kukosa hofu ya Mungu jambo ambalo ni hatari kwa viongozi na jamii kwa ujumla.

Kiongozi huyo wa imani amesema kwamba, wanasiasa sasa wamekuwa chanzo cha machafuko katika nchi zao kutokana na kuwa na tabia ya kutopenda kuachia madaraka sambamba na kukandaniza demokrasia.

Pia imeelezwa kwamba, wanasiasa wanakumbwa na tabia hiyo kutokana na kuwa na uchu wa madaraka jambo ambalo linatokana na kutokuwa na hofu ya Mungu.

Askofu Madele amesema yapo mataifa ambayo yanaingia katika machafuko kutokana na watawala wa nchi husika kukataa kutoka madarakani licha ya kumaliza muda wao.

Kiongozi huyo ametolea mfano wa rais wa Ghambia ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais na kukubali matokeo lakini muda mfupi alijitokeza na kupinga

Chanzo: Mwanahalisi
 
huyu anataka aongeze wizara, wakati sabodo anamshauri apunguze wizara, mmhh.. kaaazi kweli kweli
 
Maadili kwa watu waliopigwa upofu Wa kuona mbele ni vigumu sana kufanikiwa kwa nchi changa....Madaraka kwao ndio maisha na uhai wao....Hakuna hofu ya Mungu ndani yao....
 
Zamani wachungaji walikuwa wakiongea kila mtu anasikia, siku hizi ndio wanagombea mabar maid, kushinda kwa waganga wa kienyeji na kurushana hela na waumini wao. Hawana lolote maana wameanza mpaka kuchagua upande wa kutolea maoni yao. Kwa ujumla nafasi ya kusikilizwa na jamii wameipoteza wenyewe.
 
Uzuri wa JF mambo mengi huenda kwa facts mkuu sio vibaya kama ukatupa hilo tako alilotoa baada ya shein kupoka madaraka toka kwa Seif.

Shukran Sana.
Mkuu huyo kiongozi wa dini aliyetajwa katika uzi huu sio prominent kiasi cha kufuatwafuatwa na media, hilo moja. Lakini pili, kama ni kuzungumzia suala la Shein sio lazima azungumze na sisi hapa JF tulisome tamko lake, kwa kuwa anaweza kuwa ametamka lakini kanisani kwake katika mahubiri na hakuwepo mwandishi wa habari! Hoja yangu hapa ni kwamba hapakuwa na sababu ya kuhitimisha kuwa mtumishi huyo wa Mungu alikaa kimya baada ya goli la mkono kule Zanzibar kwa sababu tu hukumsikia!
 
Ni kweli sikumsikia mkuu na ndio mana nikaomba kama ulimsikia alichokisema sidhani kama kuna ubaya ukatujuza nasi alichokisema mkuu.

Sorry lakini kama ntakuwa nashinikiza kiongozi. Shukran sana.

Karibu.
 
Achana nae anajitoa fahamu huyo wakati Jecha alishapendekezwa kwa TUZO.
 
Ni kweli sikumsikia mkuu na ndio mana nikaomba kama ulimsikia alichokisema sidhani kama kuna ubaya ukatujuza nasi alichokisema mkuu.

Sorry lakini kama ntakuwa nashinikiza kiongozi. Shukran sana.

Karibu.
Mkuu Kioo, mimi pia sikumsikia, lakini sioni kama kutomsikia kwangu inaweza kuwa sababisho la kuhoji kwanini aseme alichosema kwa kuwa tu sikumsikia hakusema la 'goli la mkono' huko Zanzibar!
 
anatafuta ulaji huyo. yaani anashauri iundwe wizara itakayo ongozwa na kiongozi wa kiroho? sadaka na zaka haziwatoshi?
 
Basi jibu nimeshapata mkuu. Nilidhani umemsikia.
 
MAADILI kwa watumishi wa umma yameporomoka kutokana na viongozi hao kutomjua Mungu.

Ni kauli ya Christopher Madole, Askofu wa Kanisa la Gospel Ministry Jimbo la Dodoma aliyoitoa jana alipokuwa akihubiri katika kanisa hilo lililopo viwanja vya Reli mjini Dodoma.

Alikuwa akiendesha ibada ya Siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambapo amesema, umefika wakati sasa wa wanasiasa na viongozi mbalimbali serikalini kuwa na hofu ya Mungu na sio kuigiza.

“… namshauri Rais Magufuli (Rais John Magufuli) aongeze wizara moja tu ya maadili ambayo waziri wake asitokane na chama chochote cha siasa.

“Maana tunaona kuna wakati mawaziri wanaonekana kutetea vyama vyao sasa hii wizara ya maadili itakuwa inasimamiwa na kiongozi wa kiroho,”amesema Askofu Madole.

Amesema kwamba, kutokana na kuporomoka kwa maadili, mawaziri na wabunge wamekosa aibu na hata kuwa na maneno ya kashfa ndani ya Bunge.

“Kumekuwepo na maneno ya kashfa hata ndani ya bunge, mfano; mbunge anasema sizungumzi na mbwa bali nazungumza na mwenye mbwa au kusikia mbunge anasema funga milango tupigane,” amesema.

Askofu Madole amesema kuwa, yote hayo ni dalili ya watu kukosa hekima na busara na zaidi ni kukosa hofu ya Mungu jambo ambalo ni hatari kwa viongozi na jamii kwa ujumla.

Kiongozi huyo wa imani amesema kwamba, wanasiasa sasa wamekuwa chanzo cha machafuko katika nchi zao kutokana na kuwa na tabia ya kutopenda kuachia madaraka sambamba na kukandaniza demokrasia.

Pia imeelezwa kwamba, wanasiasa wanakumbwa na tabia hiyo kutokana na kuwa na uchu wa madaraka jambo ambalo linatokana na kutokuwa na hofu ya Mungu.

Askofu Madele amesema yapo mataifa ambayo yanaingia katika machafuko kutokana na watawala wa nchi husika kukataa kutoka madarakani licha ya kumaliza muda wao.

Kiongozi huyo ametolea mfano wa rais wa Ghambia ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais na kukubali matokeo lakini muda mfupi alijitokeza na kupinga

Chanzo: Mwanahalisi

Vyama vyao vipi? Wakati wote wanatoka CCM mbona Hawa viongozi hawanyooki katika kusema, labda Ni hotuba ya mwaka juzi ukiangalia content haiko updated.
 
anatafuta ulaji huyo. yaani anashauri iundwe wizara itakayo ongozwa na kiongozi wa kiroho? sadaka na zaka haziwatoshi?

uchu wa madaraka.
unafiki.
kushauri kinyume na katiba.
kupotosha waumin.

serikali haina dini.
viongozi wadini kuwa vibaraka wa wanasiasa.

(ni mtizamo tu)
 
Back
Top Bottom