Kampuni ya usafirishaji wa mizigo

Kampuni ya usafirishaji wa mizigo

Mrdash1

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,375
Reaction score
338
Wana JF nafikiria kuanzisha kampuni ya usafirishaji wa mizigo. Natarajia kupata mshiko wa kutosha kununua malori used semi trailers 3 au 4, je hili ni wazo zuri? natamani kufanya hii shughuli inanivutia sana lakini sina uzoefu nayo na sijui kama inalipa au vipi, naomba mwenye mwanga aniangazie kidogo bila dhihaka tafadhali.
 
Mimi ni transporter nipo kwenye hii field mda mrefu! Kazi inalipa ikiwa utapata contract ya mda mrefu otherwise inaumiza kichwa, running cost ni kubwa! Anyways karibu
 
karibu sana nami niko sekta hii kwa muda mrefu tangu nikiwa dereva,afisa wa usafirishaji hatimaye kuwa mmiliki,kazi inalipa kama utapata mkataba etc kama mimi nimepata mkataba WFP,shida nyingine drivers wengi sio waaminifu,karibu sana
 
Hivi nikipata toyota hiace super roof nzuri,manual disel..na kupata njia nzuri kwa kigamboni dar es salaam kama daladala iyalipa ????
 
Mimi ni transporter nipo kwenye hii field mda mrefu! Kazi inalipa ikiwa utapata contract ya mda mrefu otherwise inaumiza kichwa, running cost ni kubwa! Anyways karibu

Mkuu asante kwa mchango wako, je contract zinapatikanaje?
 
karibu sana nami niko sekta hii kwa muda mrefu tangu nikiwa dereva,afisa wa usafirishaji hatimaye kuwa mmiliki,kazi inalipa kama utapata mkataba etc kama mimi nimepata mkataba WFP,shida nyingine drivers wengi sio waaminifu,karibu sana

mawazo mazuri asante sana, sasa hii imakataba mtu utaipataje?
 
Karibu mimi pia nipo kwenye hii biashara. Kama utaisimamia mwenyewe ni biashara nzuri. Madereva asilimia kubwa sio waaminifu. Sisi wasafirishaji wadogowadogo kama tungepata njia ya kushirikiana ni rahisi kupata mikataba lakini ni kazi sana sisi kushirikiana.
 
Sisi wasafirishaji wadogo wadogo tunaweza kushirikiana lakini lazima iwe wazi tunashirikiana kwenye maeneo yapi, ili kila mmoja aweze kulinda interest zake, tunaweza kuanzisha ofisi ya umoja wa washafirishaji wadogo wadogo yenye makusudi ya kuratibu baina ya wateja na wasafirishaji, yaani inapokea maombi kutoka kwa wateja na kuyapeleka kwa kampuni za usafirishaji ambazo ziko ndani ya umoja. Hii ofisi itakuwa inakuja kampuni gani ina tenda na ipi haina
 
Asante kwa majibu mazuri. Jee nini jawabu la hawa madereva ambao sio waaminifu? Mimi nimeingia kwenye hii biashara mpaka sasa nafikiria kuiacha. Wenzetu mnafanyaje na hawa madereva?
 
Asilimia kubwa madereva wazuri na waaminifu ni kutoka iringa (wahehe)
 
  • Thanks
Reactions: 454
Back
Top Bottom