Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni wadaiwa sugu wa kodi....

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
WADAIWA SUGU WA KODI YA ARDHI WASAKWA NYUMBA HADI NYUMBA
KUKU.jpg


Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment na baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Ofisi ya Mohammed Enterprises iliyopo jingo la Golden Jubilee mara baada ya wafanyakazi wa Mohammed Enterprises kukimbia.

KUKU-1.jpg


Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.

KUKU-2.jpg


Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya kodi ya ardhi.

KUKU-3.jpg


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya serikali.

=======

Wizaraya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za za mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.

Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.

Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.

======

UPDATE:

Kampuni ya MeTL ilikanusha kwamba haidaiwi kupitia hii thread=> METL wajibu Notisi ya Malipo ya Kodi, wamesema hawadaiwi kitu
 
Ni aibu kwa mfanyabiashara mkubwa kama Dewji kukwepa kulipa kodi wakati anapata faida kubwa sana katika uwekezajj wake hapa nchini. Si kitendo cha kizalendo hata kidogo. Sheria ziboreshwe kama wenzetu walioendelea to put these people in their place
 
Ni aibu kwa mfanyabiashara mkubwa kama Dewji kukwepa kulipa kodi wakati anapata faida kubwa sana katika uwekezajj wake hapa nchini. Si kitendo cha kizalendo hata kidogo. Sheria ziboreshwe kama wenzetu walioendelea to put these people in their place
Hawezishindwa kulipa 73m wakati anawekeza Simba 20b
 
Amewekeza ili apate faida. Hiyo ni pesa yake. Lakini kodi ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na hivyo si mali yake. Anaona vigumu kulipa kodi kwa vile ni fedha inayoondoka.
 
Hapa bongo sheria nyingi inatakiwa zirejebishwe maana wageni wanabebwa sana mfano ukienda nchi za wenzetu unachombo cha moto unaambiwa chombo chako kitaenda kuzalisha carbon dioxide hivyo ulipie wakati wao wakija Tanzania hawafanyiwi hivyo e.g. in Zambia 25000 for motorcycle for a 1 period of stay 40000 for a car
 
Ni aibu kwa mfanyabiashara mkubwa kama Dewji kukwepa kulipa kodi wakati anapata faida kubwa sana katika uwekezajj wake hapa nchini. Si kitendo cha kizalendo hata kidogo. Sheria ziboreshwe kama wenzetu walioendelea to put these people in their place
Hadaiwi kodi ya ardhi ndugu, na ameshatoa hadharani receipts za malipo ya kodi ya viwanja vyote tajwa. Rejea update alioweka mleta mada.
 
Back
Top Bottom