Kampuni wamekisikitika kunijulisha kua sijafanikiwa kupenya kwenye kinyang’anyiro nilichotuma maombi yangu

Kiufagio

Senior Member
Aug 19, 2017
133
133
Habarini za muda huu wanajamvi.

Niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi bila kuwachoshaa.

Inaanza najisogeza taratibu ndani ya mwendokasi(kivukoni-moroco) ili nipate upenyo wa kutoa simu yangu mfukoni ambayo nadhani ilitetema(notification allert),

ili nijue ni ujumbe gani wa faraja napokea jioni ya leo baada ya shughuli nzito ya usambazaji CV ofisi mbalimbali katikati ya jiji hili la Chalamila.

Lahaulaaa “ We had considerable interest in the role and the quality of applicants has been extremely high. I am sorry to advise that we won’t be progressing your application further, as there are other candidates who are a closer match at this stage.”

Kumbe ilikua ni ujumbe wa email kutoka kampuni moja wakisikitika kunijulisha kua sijafanikiwa kupata uoenyo kwenye kinyang’anyiro nilichotuma maombi yangu wiki iliopita.
Nikaguna huku kijasho kikinitokaa maana mwendokasi imeshona na nimesimama.

Namalizia kushuka hili daraja la watembea kwa miguu nikifika ntamalizia.
 
Hiyo hela ya nauli inatosha kwenda bagamoyo ukanunua nanasi kibao kwa bei ya 200 hadi 500 ukazileta mbezi kwenye open space ya TANROAD na kuuza 1000 hadi 4000 mpaka msimu unaisha unakuwa na mapene ya kutosha ya kutafuta kazi bila stress!
 
nilishawai sema wasomi fresho gradu wanajiona wana akili na wabishi
 
Hiyo hela ya nauli inatosha kwenda bagamoyo ukanunua nanasi kibao kwa bei ya 200 hadi 500 ukazileta mbezi kwenye open space ya TANROAD na kuuza 1000 hadi 4000 mpaka msimu unaisha unakuwa na mapene ya kutosha ya kutafuta kazi bila stress!

Biashara kwenye daftari haijawahi muangusha mtu,
nikiona hizo vurugu za mgambo na wafanyabiashara wa mbezi luis, acha niendele kupasi hili shati langu kauka nikuvae na bahasha ya 200 ambayo kwa wiki nabadilisha mara tatu inakua 600 kazi inaendelea.
 
"E="Kaka yake shetani, post: 49224410, member: 697685"]
ikifika miaka 5 utaanza kuona wanaomaliza vyuo ni wajinga
[/QUOTE]" umenikumbusha mbali xana
 
Back
Top Bottom