Aisee hii kitu inanishangaza sana. Wengine huwarekodi hata wapenzi wao wakiwemo wake zao na kisha kuweka mtandaoni. Sijui wanapata faida gani kwa kuwarekodi wenzao bila ridhaa zao na kuwadhalilisha kwenye kadamnasi. Kama mtu ameridhia kurekodiwa na kuwekwa mtandaoni hilo sina tatizo nalo.