Kambi ya Upinzani isione aibu kumuunga mkono Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
KILA ninapoangalia utendaji wa Rais John Magufuli ninakumbuka maneno ya aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Leonard Kanango Shayo kwamba, “tukichagua viongozi wazuri, tutakuwa tumeshinda uchaguzi, tukichagua viongozi wabovu, tutakuwa tumeshindwa uchaguzi”.

Kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria na kuonesha kwa vitendo nia ya kuleta mabadiliko ya kweli, ni wazi Watanzania wameshinda uchaguzi kwa kuchagua viongozi wazuri. Ninaandika makala haya nikiwa ni mwanasiasa kutoka Kambi ya Upinzani, Chama cha NCCR-Mageuzi. Hata hivyo, makala yangu hayana uhusiano na wala siyo msimamo wa chama hicho wala Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Makala haya ni mtazamo wa raia huru na ambaye yuko huru kuwa na mawazo na kutoa mawazo hayo kwa watu wengine. Mwandishi wa makala haya, hana sababu yoyote ya kuzuia mawazo haya kuazimwa au kuchukuliwa na taasisi yoyote ikwemo NCCR-Mageuzi na hata UKAWA kama itaonekana inafaa. Wakati mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalemdo, Anna Mghwira , anajiandaa kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema, “Wenye hekima wakinyamaza, wapumbavu huongezeka.”

Nia ya Mghwira ni kuwahamasisha watu wenye hekima kujitokeza na kugombea nafasi za uongozi na kupaza sauti kukemea vitendo vya rushwa, ufisadi pamoja na kuimarisha mihimili ya kusimamia haki na nidhamu ili kuitoa Tanzania kwenye lindi la umasikini. Ninaandika makala haya nikiwa na ufahamu wa kutosha kuwa, baadhi ya vyama vya siasa na wagombea walikuwa kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.

Wapo walioshindwa au kushinda kwa uhalali, lakini pia yapo madai kuwa wapo walioshinda au kushindwa kwa uharamu, hatua gani basi zichukuliwe hilo siyo kusudio la makala ya leo. Mwandishi wa vitabu Marekani , Jack Confield, anasema, ”Usiwe na wasiwasi kuhusu kushindwa, kuwa na wasiwasi na nafasi unazopoteza kwa kuogopa kujaribu”. Naye, mchezaji maarufu wa zamani wa mpira wa kikapu, Michael Jordan amepata kusema, “Ninakubali kushindwa, lakini kamwe sitakubali kutojaribu tena.

Hakuna mtu ambaye hajawahi kushindwa jambo katika maisha yake”. Nimeyarejea maneno ya watu hawa, kama sehemu ya faraja ya dhati kwa wagombea wote walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita na kuwahimiza wajiandae kwa chaguzi nyingine kwa kuzingatia usemi, “Asiyekubali kushindwa sio mshindani.” Watanzania wametathmini kila kona kuwa Rais Magufuli ni kiongozi mzuri hivyo waliamua kumchagua na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.

Rais Magufuli amekuja na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”. Binafsi nimeipenda kaulimbiu hiyo na bila kutafuna maneno ninampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya hadi ninapoandika makala haya. Ninaamini, kuwa Rais Magufuli siyo mwizi wala siyo mlafi. Anatambua mahitaji ya msingi ya Watanzania kuwa ni kuondoa kero ya rushwa, kupambana dhidi ya ufisadi, kuboresha huduma za afya, elimu na kuhakikisha vyombo vya sheria vinatoa haki bila upendeleo.

Ninaandika makala haya nikiwa na kiu kubwa ya kuona Watanzania wenye nia njema na nchi yao wakimsaidia Rais Magufuli katika kutimiza wajibu wake wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia Kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu.” Naamini kwamba chama chochote cha upinzani chenye nia njema na Watanzania kinaomba Rais Magufuli aongeze kasi yake ya ‘kutumbua majipu’ kwa kufukua maovu na kuyakomesha ili kujenga nidhamu na utamaduni wa kulitumikia Taifa badala ya kutumikia maslahi binafsi.

Hata hivyo ninafahamu kuwa kama Rais Magufuli ataendelea na kasi yake ya ‘kutumbua majipu’ baadhi ya vyama vya siasa na hasa vyenye mitazamo finyu na hafifu na ambavyo havitaweza kuendana na kasi ya mabadiliko vitafutika katika uso wa dunia ya wapenda mabadiliko ya kweli. Kama kasi hii ya Rais Magufuli, Tanzania inatakiwa kuwa na vyama makini na vyenye viongozi makini kwa kuwa Watanzania wataenda kupiga kura kwa wagombea wanaofaa tofauti na mazoea ya kuwapigia kura wagombea tunaowapenda hata kama hawafai kuwa viongozi.

Wakati analihutubia Bunge, pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli aliwaomba wabunge wamsaidie katika wajibu wake wa kupambana na maovu na kushirikiana naye kuleta maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali tofauti za vyama. Naamini hakuna chama makini cha siasa kitazuia wabunge wake kumsaidia Rais katika vita hii. Mwanasaikolojia na mwanafizikia wa zamani wa Ujerumani, amepata kusema Albert Einstain , “ Dunia ni sehemu hatari ya kuishi, siyo kwa sababu ya watu wake kuwa waovu, bali kwa sababu ya watu wasiochukua hatua kuhusu huo uovu.”

Nimeazima maneno haya, kuvitahadharisha baadhi ya vyama vya siasa vinavyodhani kuwa , uwepo wake unategemea kasoro za chama tawala zinazosababishwa na utendaji hafifu serikalini. Hivi sasa Rais Magufuli anatekeleza kwa vitendo dhana ya utawala bora, unaozingatia misingi ya sheria na katika uongozi wake tumeshuhudia jinsi anavyozingatia sheria na maadili ya uongozi, kuwakosoa ama kuwaondoa madarakani viongozi ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao.

Baadhi ya vyama vya siasa vina ufahamu mdogo juu ya dhana ya uongozi, viongozi na wanachama wetu wanadhani viongozi ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu. Mwanafalsafa maarufu wa China, Lao Tzu aliyetawala katika karne ya sita, alizungumzia dhana halisi ya kiongozi kuwa ,”Kiongozi bora na mwema ni yule ambaye watu hawatambui mara moja kwamba yu miongoni mwao, ni yule ambaye majukumu yake yakiisha kukamilika na malengo yake yakishakutimia, watu watasema, tumepata mafanikio haya kwa juhudi zetu wenyewe”.

Naye, John Quincy Adam, Rais wa sita wa Marekani amewahi kusema “Kama matendo yako yanavutia wengine kuwa na ndoto zaidi, kujifunza zaidi, kufanya kazi zaidi na kukua zaidi, basi wewe ni kiongozi”. Rais Magufuli ameonesha kwa vitendo kuwa yeye ni kiongozi ambaye anataka kutimiza malengo yake ya kuleta mabadiliko na maendeleo ya kweli pasipo kuyumba wala kuyumbishwa na kundi lolote.

Ni kiongozi mwenye msimamo na asiyependa kujikweza wala kutumia fedha za walipa kodi kwa mambo ya anasa badala yake anaelekeza fedha zitumike kwa manufaa ya watu wote na kwa faida ya muda mrefu kama vile kuboresha huduma za afya, upanuzi wa barabara na kuwekeza katika elimu. Hivyo viongozi ndani ya Serikali na hata kambi ya upinzani inapaswa kubadili mwenendo ili kwenda na kazi ya Rais Magufuli.

Viongozi waliokuwa wameelekeza mikakati yao kwenye kukosoa kila kitu kinachofanywa na Serikali sasa wanapaswa kujipanga upya maana tayari Dk Magufuli anafanya hata yale ambayo hawakufikiria kuyakosoa. Baadhi ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa miaka ya 90 kikiwemo Chama Cha Mapinduzi vikiwa sasa na umri mkubwa na unaotosha kufanya tathmini yakinifu.

Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini, Miriam Makeba amewahi kusema, “Umri mkubwa ni kitu cha kujivunia maishani. Kwani unakuwezesha kujua namna zote dunia inavyogeuka ili kama huwezi kugeuka nayo basi uweze kuipisha isije ikakuponda wakati inageuka”. Rais Magufuli anakiwezesha chama chake cha CCM kwenda na wakati na kugeuka sanjari na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ili kisipondwe na kuwekwa chini na wanamageuzi wanaotaka kuona Tanzania yenye viongozi waadilifu na wenye nia ya kuleta maendeleo ya kweli kwa watu wote.

Watanzania na hasa WanaCCM wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli ili kutimiza yale yaliyosemwa na Mwenyekiti wa Chama na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye amewahakikishia Watanzania kuwa chama hicho kiko bega kwa bega na Rais Magufuli katika kufichua na kukomesha uvundo wa maovu yanayotendwa na viongozi wa serikali.

Mwandishi wa Makala haya ni Faustine Sungura, Mkuu wa Idara ya Kampeni na uchaguzi wa NCCRMageuzi
 
Kweli kabisa, wampe ushirikiano wa kutosha kwa kuunga mkono hatua zenye maslahi mapana kwa taifa na pia kuonesha majipu yalipo, na pale wanapoona majipu ya wazi yanapuuziwa wasisite kupaaza sauti zao mpaka zisikike. Ila pia wawe "watch dogs" kuhakikisha haki za raia haziminywi!
 
Wataungaje mkono wakati wao ni wapinzani!
Lini simba waliiunga mkono yanga

Tatizo hilo jina la vyama vya upinzani limejaa mapepo ya upinzani ndani yake ndio maana wapinzani huwa wamejaa mapepo ya kupinga tu.Wenzetu vyama vyao mfano Raisi akishinda hawasiti kumpongeza hadharani na pia akifanya vizuri huwa wanawapongeza hadharani.

Kwa Tanzania kuna wachache wa vyama vya upinzani wanajitambua lakini wengine hata uwalipie watoto wao ada, uwape mikopo elimu ya juu watoto wao utakuta wamebaki kupinga tu sababu wamejaa mapepo ya upinzani kwenye roho zao.

Wote wenye mapepo ya upinzani dhidi ya kila Kinachofanywa na serikali mapepo ya upinzani yaliyowajaa na yawatoke kwa Jina la Yesu na yasiwarudie tena.Semeni AMEN ILI PEPO WENU WATOKE CHAP CHAP.
 
Marehemu Abbas Gulamali akiwa mwenyekiti wa Yanga.alipoulizwa kwa nini Yanga hawakuishangilia simba itwae kombe la Africa alijibu "Uzalendo umetushinda"
 
hivi kabisa kutoka moyoni unaona magufuli yuko serious 100% kupambana na mafisadi!!!ataifishe mali za magumashi za mwinyi,mkspa na jk...unacheza wewe mtoa mada
 
Back
Top Bottom