Kamati za harusi ni shiida!

Kamati za harusi ni shiida!

mcmzungu

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
48
Reaction score
66
Naitwa MC SIMON Mzungu ni mshereheshaji (MC) katika harusi,send off na matukio mbalimbali,mara nyingi Nimealikwa katika vikao mbali mbali vya harusi lakini Washereheshaji Tunaulizwa maswali meeengi magumu na kamati mbalimbali za harusi kama Tutalipwa mamilioni ya fedha,MC Unaulizwa Utatupa offer gani au changia mchango upate kazi,binafsi Naamini MC Natakiwa kutoa huduma bora na nzuri,binafsi kauli mbiu yangu (huduma bora yenye hadhi ya nyota tano daima) Najitosheleza kwa huduma nzuri japo ni Mshereheshaji (MC) ambaye naanza.Wadau ambao ni wanakamati je?MC kama MC Luvanda,MC Mambya,MC Kibonde na MC Godwin Godwe huwa Mnawaweka kikaangoni kwenye kamati zenu za harusi kwamba watawapa offer gani?champagne au kuchangia sherehe?karibuni Nasubiri maoni.
 

Attachments

  • 1440171475082.jpg
    1440171475082.jpg
    13.7 KB · Views: 707
Ukishalijua soko si uwe ba mkakati wa kupambana? Mfano kama fee yako ni 700,000 utaiambia kamati malipo ni 750,000 ila 50 itakuwa mchango wako wao wakupe 700

Etc etc

Ila kama promo unayojipigia ndio hii wateja utawakosa
 
toa ndiyo upate michongo zaidi sasa hiv bdo mchanga sana,jitangaze kwa kujitoa kwanza bdae utaona matunda yake
 
tunaacha kufunga harusi na kuchangia send offs.
tafuteni kazi nyingine ya kufanya.
 
sa ndo kwanza unaanza afu unakua mgumu kujilinganisha na kuvanda... ata wakikwambia uchangie double toa tu mkuu, ukifika unapga kazi ya ukweli watu wengine zaidi wakujue!!! mwanzo mgumu
 
asanteni sana Wadau kama Badili tabia,Kaka yako Napita,Nyalotsi na Junior Cux asanteni sana Sijilinganishi na MC Luvanda,He is the best,Sisi chipukizi mkitupa mawazo mazuri hakika Mtaibua vipaji vipya Mungu awabariki.
 
We uje kivingine kabisa mkuu, uwe unawapa offer ya kuwanengulia masebene ya kufa mtu kama mc flani hivi wa kanda ya ziwa ambae cpendi kumtaja jina uone kama utakuwa unakosa kazi
 
Back
Top Bottom