Kamati ya Zitto yamhoji CAG

Kamati ya Zitto yamhoji CAG

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Zitto-kabwe--November20-2014.jpg

Zitto Kabwe,Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeanza kazi ya kuchambua ripoti za uchunguzi wa kashfa ya kuchota fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku ulinzi mkali unaohusisha askari wa Jeshi la Polisi wenye silaha za moto na makachero ukiwa umeimarishwa.

Mbali na kuchambua ripoti za uchunguzi huo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), PAC inatumia fursa hiyo pia kuwahoji wahusika wote waliohojiwa na taasisi hizo wakati wa uchunguzi wao.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE ilizipata mjini hapa jana zinaeleza kuwa wa kwanza kuhojiwa na PAC alikuwa ni Kaimu CAG, Francis Mwakapalila.

Mahojiano kati ya PAC na Mwakapalila yalianza saa tano asubuhi na hadi tunakwenda mitamboni yalikuwa bado yanaendelea.Ulinzi wa askari hao uliimarishwa siyo tu kwa watu baki, bali hata kwa wajumbe wa PAC.

Kila mjumbe wa PAC aliyefika katika ukumbi unaotumika kwa kazi hiyo, alikuwa akizima simu yake na kisha anaikabidhi kwa askari polisi, ambao pia walikuwa wanadhibiti hata wageni waliokuwa wakifika eneo la ukumbi wa kikao hicho.

Waandishi wa habari, ambao walifika jana katika jengo la Hazina, ambako PAC inalitumia kufanya kazi hiyo, kwa lengo la kufuatilia ahadi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, ya kuzungumza nao, lakini walizuiwa na askari hao.

Wakati wabunge hao wakitoa tuhuma hizo nzito kwamba serikali inatumia mahakama kuzuia Bunge kufanya kazi yake, hali ya ulinzi nje ya ukumbi wa Chuo cha Mipango inakokutana Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuchambua ripoti ya Escrow ilikuwa imeimarishwa, wakiwapo polisi wenye bunduki.

PAC Jumatatu wiki hii walikabidhiwa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Escrow na inatarajiwa kuiwasilisha bungeni Jumatano wiki ijayo.

Mwandishi wa NIPASHE mjini Dodoma alishuhudia polisi wenye silaha nje ya ukumbi huo, hali iliyoashiria kwamba watu wengine mbali na wajumbe wa kamati na waliokuwa wanaitwa kwa mahojiano hawakuhitajika kufika eneo hilo.

Hali ya ulinzi ikiwa ni ya kuogofya na baada ya kuzuiwa, waandishi walituma ujumbe kwa Zitto kupitia kwa mmoja wa maofisa wa Bunge, kwamba wamefika katika jengo hilo ili awaeleze yaliyokwishajiri na yanayoendelea kujiri.

Afisa huyo wa Bunge alipokea ujumbe huo na kuingia katika ukumbi wa jengo hilo ambako PAC inaendelea na kazi yake, baada ya dakika chache, alirudi na jibu alilodai kuwa linatoka kwa Zitto kwamba, amesema wako kazini na kwa hiyo hawezi kutoka kwa ili kuzungumza na wanahabari. Hali hiyo iliwalazimisha wanahabari kuondoka eneo hilo.

Zitto alikuwa ameahidi kwamba angekutana na wanahabari jana kwa ajili ya kuwapatia taarifa kuhusiana na mchakato wa kuwahoji wahusika wa sakata la kuchotwa kwa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kwenye akaunti hiyo katika mazingira yenye utata.

Jumatatu wiki hii, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliikabidhi ripoti ya uchunguzi ya CAG kwa PAC kwa ajili ya kuipitia na kuwahoji watu kadhaa kabla ya kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa na Wabunge.

CHANZO: NIPASHE
 
Wakifikia zamu ykumhoji wanashasheria mkuu Jaji WAREMA Zitto akae mbali vinginevyo anaweza kumrukia na kumkaba shingoni , vile vile ikifikia zamu ya kumhoji Katibu mkuu wa Nishati na Madini Mh Eliakim Maswi Zitto ajihadhari.
 
Bilioni 300...hizi pesa ukizipanga noti moja moja barabarani kutoka Ubungo dar..zinaishia Chalinze.
 
Nimejaribu kutatafuta majina ya wajumbe wote wa PAC nimeshindwa kuwapata ukiacha huyo Zitto na makamu wake Fulikunjombe. Jee wengine ni wakina nani? Ni vema tuwajue maana kama kamati itafanya usaliti tusiishie kumtuhumu Zitto kama vile yuko peke yake katika maamuzi. Mwenye nayo atuwekee.
 
Nasikia Aden Rage yumo.
 
Billioni 300 na bado tunasema nchi masikini!!
Sijui tugome na kuchangia hela za maabara??!!
 
Zitto-kabwe--November20-2014.jpg

Zitto Kabwe,Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeanza kazi ya kuchambua ripoti za uchunguzi wa kashfa ya kuchota fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku ulinzi mkali unaohusisha askari wa Jeshi la Polisi wenye silaha za moto na makachero ukiwa umeimarishwa.

Mbali na kuchambua ripoti za uchunguzi huo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), PAC inatumia fursa hiyo pia kuwahoji wahusika wote waliohojiwa na taasisi hizo wakati wa uchunguzi wao.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE ilizipata mjini hapa jana zinaeleza kuwa wa kwanza kuhojiwa na PAC alikuwa ni Kaimu CAG, Francis Mwakapalila.

Mahojiano kati ya PAC na Mwakapalila yalianza saa tano asubuhi na hadi tunakwenda mitamboni yalikuwa bado yanaendelea.
Ulinzi wa askari hao uliimarishwa siyo tu kwa watu baki, bali hata kwa wajumbe wa PAC.

Kila mjumbe wa PAC aliyefika katika ukumbi unaotumika kwa kazi hiyo, alikuwa akizima simu yake na kisha anaikabidhi kwa askari polisi, ambao pia walikuwa wanadhibiti hata wageni waliokuwa wakifika eneo la ukumbi wa kikao hicho.

Waandishi wa habari, ambao walifika jana katika jengo la Hazina, ambako PAC inalitumia kufanya kazi hiyo, kwa lengo la kufuatilia ahadi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, ya kuzungumza nao, lakini walizuiwa na askari hao.

Wakati wabunge hao wakitoa tuhuma hizo nzito kwamba serikali inatumia mahakama kuzuia Bunge kufanya kazi yake, hali ya ulinzi nje ya ukumbi wa Chuo cha Mipango inakokutana Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuchambua ripoti ya Escrow ilikuwa imeimarishwa, wakiwapo polisi wenye bunduki.

PAC Jumatatu wiki hii walikabidhiwa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Escrow na inatarajiwa kuiwasilisha bungeni Jumatano wiki ijayo.

Mwandishi wa NIPASHE mjini Dodoma alishuhudia
polisi wenye silaha nje ya ukumbi huo, hali iliyoashiria kwamba watu wengine mbali na wajumbe wa kamati na waliokuwa wanaitwa kwa mahojiano hawakuhitajika kufika eneo hilo.

Hali ya ulinzi ikiwa ni ya kuogofya na baada ya kuzuiwa, waandishi walituma ujumbe kwa Zitto kupitia kwa mmoja wa maofisa wa Bunge, kwamba wamefika katika jengo hilo ili awaeleze yaliyokwishajiri na yanayoendelea kujiri.

Afisa huyo wa Bunge alipokea ujumbe huo na kuingia katika ukumbi wa jengo hilo ambako PAC inaendelea na kazi yake, baada ya dakika chache, alirudi na jibu alilodai kuwa linatoka kwa Zitto kwamba, amesema wako kazini na kwa hiyo hawezi kutoka kwa ili kuzungumza na wanahabari. Hali hiyo iliwalazimisha wanahabari kuondoka eneo hilo.

Zitto alikuwa ameahidi kwamba angekutana na wanahabari jana kwa ajili ya kuwapatia taarifa kuhusiana na mchakato wa kuwahoji wahusika wa sakata la kuchotwa kwa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kwenye akaunti hiyo katika mazingira yenye utata.

Jumatatu wiki hii, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliikabidhi ripoti ya uchunguzi ya CAG kwa PAC kwa ajili ya kuipitia na kuwahoji watu kadhaa kabla ya kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa na Wabunge.

CHANZO: NIPASHE
Sikia Mkuu, ninavyoifahamu Danganyika....Ooops sorry, I mean, Tanganyika hii, hayo magobole, mitutu inayozunguka-zunguka nje ya hiyo nyumba, ni changa la macho tu. Hizo ripoti za uchunguzi wa kashfa ya kuchota matrillioni ya Escrow, zime twistiwa in a very very high technik, itawasumbua sana mi nakwambia.
kumbuka EPA, MEREMETA< etc sijui !
 
Wakifikia zamu ykumhoji wanashasheria mkuu Jaji WAREMA Zitto akae mbali vinginevyo anaweza kumrukia na kumkaba shingoni , vile vile ikifikia zamu ya kumhoji Katibu mkuu wa Nishati na Madini Mh Eliakim Maswi Zitto ajihadhari.

Acha ushabiki kilaza wewe, wewe unafikiri wote wavuta ndumu kama wewe. Vitoto vilivyokulia mazingira hatarishi vinamatatizo sana!
 
Sikia Mkuu, ninavyoifahamu Danganyika....Ooops sorry, I mean, Tanganyika hii, hayo magobole, mitutu inayozunguka-zunguka nje ya hiyo nyumba, ni changa la macho tu. Hizo ripoti za uchunguzi wa kashfa ya kuchota matrillioni ya Escrow, zime twistiwa in a very very high technik, itawasumbua sana mi nakwambia.
kumbuka EPA, MEREMETA< etc sijui !

Dahhhhhh!!! Tulisema wakuu, Daahhhh! VILIO VYA KUCHAKACHUA RIPOTI VIMEANZA HUKU, Dahhhhhh! Tulieni hizi mbwembwe za kulialia na ripoti za nini?? Subiri ripoti iwekwe mezani tarehe 26, wewe umeshaiona ripoti yenyewe mpaka useme kuna uchakachuaji? MLIPANGA MATOKEO YA KUWAFURAHISHA NYINYI KUMBE!
 
Nimejaribu kutatafuta majina ya wajumbe wote wa PAC nimeshindwa kuwapata ukiacha huyo Zitto na makamu wake Fulikunjombe. Jee wengine ni wakina nani? Ni vema tuwajue maana kama kamati itafanya usaliti tusiishie kumtuhumu Zitto kama vile yuko peke yake katika maamuzi. Mwenye nayo atuwekee.

Angalia kwenye tovuti ya bunge.
 
Back
Top Bottom