Kamati ya uongozi CUF yamtaka Lipumba agombee kuepusha mpasuko

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,842
43,296
Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli usio pingika tangu aondoke Prof Lipumba cham cha CUF kimeyumba kabisa na kukosa kujisimamia na kutegemea maamuzi ya UKAWA hasa CHADEMA!

Kurejea kwa Lipumba kunaweza kuleta mpasuko mkubwa sana kwakuwa kuna kundi kubwa la wanachama lina muhitaji huku kukiwa na kundi dogo lililo karibu na UKAWA likishawishiwa kuto mruhusu kugombea uenyekiti!

Hata hivyo Mh Prof Lipumba mwenye wafuasi wengi ndani ya chama amesisitiza kugombea nafasi hiyo inayo muhitaji!

Leo hii mwenyekiti wa kamati ya uongozi Bwana Twaha amemsihi Mh Lipumba kugombea nafasi ya uenyekiti ili kukinusuru chama na mpasuko ambao umeanza kutokea!

======

CHAMA cha wananchi CUF kimesema mkutano mkuu wa taifa ambao unategemewa kumpata Mwenyekiti wa chama hicho, upo pale pale, na kuweka msimamo kuhusu Ibrahimu Lipumba kuwa kama anataka kurejea katika nafasi yake achukue fomu. Tamko hilo ni kufuatia sintofahamu kwa wanachama wa chama hicho kuwa huenda mkutano mkuu usiwepo kutokana na ujio wa ghafla wa Prof. Ibrahim Lipumba aliyekua Mwenyekiti wa chama ambaye alijiudhuru cheo hicho.

Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho amesema tayari fomu za ugombea zimeshapelekwa katika ofisi ya wilaya tayari kwa kujazwa.
“kuanzia 1 Julai washiriki katika ngazi ya Mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa chama pamoja na Makamu mwenyekiti wachama hicho na wataanza kuchukua fomu hadi Julai 20,” amesema.

Amesema, 21 Agosti baada ya zoezi la ujazaji fomu kukamilika, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Kitaifa watakaa kuchagua viongozi hao katika ukumbi wa Land Mark Ubungo Jijini Dar es Salaam. Lipumba alijiudhuru katika kipindi cha uchaguzi Mkuu 25 Oktoba kutokana na sababu aliyoitoa kuwa ni uwepo wa aliyekua Mgombea urais, Edward Lowassa kuwa alihamia kwenye chama kwa kutofuata utaratibu.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema kutokana na katiba ya chama, Lipumba hatakiwi kurudi katika nafasi hiyo kwa kutengua kujiuzulu kwake ispokuwa ni kama anahitaji nafasi hiyo achukue fomu upya kugombea nafasi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Taifa.


Chanzo: Mwanahalisi Online
 
CUF wanatakiwa kuwa msimamo kutomuruhusu huyu mamluki kugombea uenyekiti huyo ametumwa kufanya kazi maalumu.
 
Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli usio pingika tangu aondoke Prof Lipumba cham cha CUF kimeyumba kabisa na kukosa kujisimamia na kutegemea maamuzi ya UKAWA hasa Chadema!

Kurejea kwa Lipumba kunaweza kuleta mpasuko mkubwa sana kwakuwa kuna kundi kubwa la wanachama lina muhitaji huku kukiwa na kundi dogo lililo karibu na UKAWA likishawishiwa kuto mruhusu kugombea uenyekiti!

Hata hivyo Mh Prof Lipumba mwenye wafuasi wengi ndani ya chama amesisitiza kugombea nafasi hiyo inayo muhitaji!


Leo hii mwenyekiti wa kamati ya uongozi Bwana Twaha amemsihi Mh Lipumba kugombea nafasi ya uenyekiti ili kukinusuru chama na mpasuko ambao umeanza kutokea!
View attachment 357332
Mnafiki mkubwa sasa CUF kuyumba ndo furaha yenu nyie CCM?
 
siaza za tanzania ni za kipuuzi sana.twaha taslima naye kashafika bei
 
Napingana na wewe, Lipumba hana umakini wowote, Huwezi kujiuzulu kwa sababu alizozitaja, halafu uombe kurudi ilhali sababu alizozitaja bado ziko pale pale.
Sasa amehamua kurudi na wanachama wamemkubali hakuna wenye chama zaidi ya wana chama!
 
Lumumba at work....propaganda....Cuf wakimruhusu Huyo Prof. wataanguka kisiasa ni heri wajilipue kama cdm walivyofanya kwa Dr. Slaa.
Hakuna propaganda bali CUF wana mhitaji wenyewe na walimbembeleza...
 
Sasa amehamua kurudi na wanachama wamemkubali hakuna wenye chama zaidi ya wana chama!
Wanachama wapi?Acha porojo zako na Propaganda za kitoto. Uongozi hauamuliwi hivyo! Uamue kujiuzulu katikati ya vita halafu uamue kurudi baada ya ushindi?
 
Back
Top Bottom