Kamati ya Ulinzi na Usalama Yamjia Juu Mwekezaji Mkoani Manyara

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kamati ya ulinzi na usalama kanda ya kaskazini imemwagiza mwekezaji wa mgodi wa kampuni ya Tanzanite iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, kuwarudisha kazini haraka wafanyakazi zaidi ya 200 kisha kuwalipa stahiki zao kufuatia mwajiri kukiuka sheria na taratibu za kazi nchini.

Akizungumza na waathirika wa kampuni hiyo walioandamana hadi kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanajro ambaye pia na mweneykiti wa kamati ya ulinzi na usalama kanda ya kaskazini Amosi Makala amesema walishakubaliana katika kikao cha pamoja kilichoshirikisha wakuu wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuwa lazima mwekezaji azingatie sheria na taratibu za kazi na sio kukanyaga sheria za nchi.

Wakielezea changamoto zilizopo katika mgodi huo na jinsi wanavyokabiiana nazo, baadhi ya waathirika wa mgodi huo unaoendeshwa na wageni kwa kushirikiana na wazawa walioingia ubia na serikali, wamesema hawamtaki mwekezaji huyo kwa sababu anajali maslahi yake na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanadai haki zao ikiwemo mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF pamoja na mishahara.

Kufuatia hatua hiyo, mwekezaji wa mgodi huo wa Tanzanite Feisal Chabay amekiri kuwafukuza kazi wafanyakazi zaidi ya 200 amedai kuwa walikika wao sheria za kazi kwa kuweka mgomo wakidai stahiki zao hatua ambayo ni ukiukwaji wa sheria za kazi kwa sababu madai yanataratibu zake za kuyadai na sio kugoma kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom