Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kigamboni imetembelea vivuko vyake

Hivi kwa nin mnapenda kumuachia Mungu kila jambo? Hili nalo la kumuachia Mungu kweli? Alikupa Ufahamu na Utashi wa kazi gani?

Kwa namna hii umasikini utaisha Afrika kweli!?
Sasa tufanye nini zaidi ya kumuomba Mungu? Maana hiyo serikali na wahusika wa usafiri wa majini hawajifunzi kutokana na makosa ya nyuma. Hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa za kuepusha au kupunguza madhara ajali hizi zitokeapo.
Acha sisi waamini tubaki kumwomba Mungu atuepushie mbali na haya majanga hatuna namna nyingine.
 
Huu upuuzi wa kusubiri mpaka majanga yatokee ndipo wanafanya ziara za kushtukiza ni unafiki wa hali ya juu
 
Leo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kigamboni imetembelea vivuko vyake na kubaini changamoto tatu kuu na za msingi
1. Kutokuwepo kwa namba ya dharura kwenye vivuko
2. Tv za sehemu ya kusubiria abiria kutofanya kazi
3. Kutokuwepo kwa CCTV camera.
Najiuliza kweli hizi ndizo changamoto za msingi?
 
Kamati yenyewe ina watu wenye uelewa wa masuala husika? Hili ndilo tatizo la nchi yetu. Wanasiasa ndiyo wataalam wa kila kitu. Hivi hakuna mamlaka zenye wataalam zinazisimamia hivyo vyombo? Mpaka wiki mbili ziishe tutaona na kusikia kila sarakasi na kila tamko. Mwezi ukiisha kila mtu amesahau!
 
Walikua wapi siku zote ? kama leo hii wamegundua kasoro zote hizo na bado hawaoni nyingine ambazo zipo kibao, na wao washughulikiwe
 
Hivi kwa nin mnapenda kumuachia Mungu kila jambo? Hili nalo la kumuachia Mungu kweli? Alikupa Ufahamu na Utashi wa kazi gani?

Kwa namna hii umasikini utaisha Afrika kweli!?
Nashangaa, utafikiri Mungu ndie anaekatisha tiketi za ferry na kupakia zaidi ya uwezo wa vivuko
 
Siku zote hizo alikuwa wapi yani mpaka ajali itokee ndio ajiongeze viongozi Hawa ni mizigo
 
Mh Rais ana pata tabu na watendaji wetu Lakini watanyooka mpaka waelewe nidhamu ya kazi kuakikisha usalama wa ferry ni wajibu kila siku Rais ana bebeshwa mizigo ambayo kwa uzembe wa mtu aliyesa hau majukumu yake
 
Back
Top Bottom