M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,026
Tangu ateuliwe kwenye nafasi aliyo nayo sasa, nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana huyu kamanda Siro, kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
Anaonekana anachagua maneno sahihi kwa wakati sahihi. na mahali sahihi. na kwa hadhira sahihi.
Halikadhalika huwaga hakurupuki katika namna anavyotekeleza majukumu yake. Mfano ni namna anavyolishughulikia suala la kuondolewa kwa ombaomba jijini Dar (soma hapo chini).
Bahati mbaya sana sijui ufanisi wake kabla ya hii nafasi yake ya sasa lakini based on what am seeing now, safely niwaweza kumtabiria kuwa anaweza kuwa mmoja wa viongozi wakuu serikalini huko siku za mbeleni. maybe PM or even prezidaa. I mean akiendelea kuwa na umakini huu huu anaounyesha sasa.
Time will tell. Definitely.
========================================================
Mkakati wa Makonda kuondoa ombaomba ‘waingia mdudu’
Kwa ufupi
Kamanda Sirro asema zinahitajika fedha za kuwasafirisha na chakula
By Pamela Chilongola na Colnely Joseph, Mwananchi pchilongola@mwananchipapers.co.tz
Dar es Salaam. Mpango wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wa kuwakamata ombaomba katikati ya jiji umekwama kutokana na polisi kudai kuwa baadhi ya taratibu za haki za binadamu zinapaswa kufuatwa.
Aprili 12, Makonda alitangaza kufanya operesheni ya kuwaondoa ombaomba hao waliozagaa katikati ya jiji kuanzia jana.
Ombaomba hao husababisha usumbufu kwa waendesha magari na waenda kwa miguu kwani hukaa kando ya barabara kuu huku wakiomba misaada na wengi wao wana sehemu za kuishi na wengine wanadaiwa kuwa na familia zao.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema kazi ya kuwakamata haijaanza kama ilivyoagizwa na mkuu huyo wa mkoa kwa sababu wanasubiri kukamilishwa kwa utaratibu huo wa haki za binadamu.
Sirro alisema watakapowakamata wanatakiwa kuhifadhiwa na wapatiwe chakula. “Pia tunahitaji fedha kwa ajili ya kuwasafirisha kuwarudisha kwenye mikoa wanakotoka, tunaifanya kazi hii kwa kushirikiana na wenzetu wa Ustawi wa Jamii na mipango itakapokamilika tutaifanya kazi hii mara moja,” alisema.
Hata hivyo, Sirro alisema operesheni hiyo itakapoanza itakuwa endelevu na siyo nguvu ya soda kama baadhi ya watu walivyoanza kuvumisha.
Alisema Jeshi la Polisi ni wasimamizi wa sheria, hivyo wamelazimika kufikiria suala hilo katika mazingira ya kibinadamu.
Kamanda Sirro alisema baadhi ya ombaomba wametii sheria na wameanza kuondoka na kutoa wito kwa waliobaki waondoke kwa hiyari badala ya kusubiri kukamatwa.
Mwananchi ilitembelea maeneo ya katikati ya jiji ikiwamo ya Stendi ya Posta na kujionea idadi ndogo ya ombaomba wakiendelea na kazi hiyo tofauti na ilivyozoeleka.
Mmoja wa ombaomba hao, Edina Ambros alisema ataendelea kuomba kwa sababu ni mlemavu kwani hana kazi ya kumuingizia kipato. Aliilaumu Serikali kwa madai imeshindwa kusikiliza kilio chao cha kusaidiwa.
“Leo nipo peke yangu wenzangu wamejificha na sijui walipo, lakini mimi nitaendelea kukomaa hapahapa sababu sina namna nyingine ya kupata riziki,” alisema Ambrose.
Ombaomba mwingine aliyekataa kujitambulisha jina, alisema anatumia stahili ya kuomba akiwa ameshika mzani ili asibainike.
“Nimeamua kuweka mzani huu kwa kuhofia kukamatwa, anapotokea mtu namuomba anisaidie kwa chochote alichokuwa nacho,” alisema.
Source: MWANANCHI (Jumanne 19 Aprili 2016)