Kamanda Simon Sirro awaonya wanasiasa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka wanasiasa wanaosababisha kutokea vurugu kutambua kuwa Polisi wapo na watawachukulia hatua wote wanaohusika kusababisha vurugu ambazo zinaweza kusabisha upotevu wa amani nchini.

Kamanda Sirro aliyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa baadhi ya wanachama wa moja ya chama cha siasa katika uchaguzi wa meya wa jiji la Dar es Salaam uliofanyika jana jumamosi.

Alisema hakuna mwanasiasa aliye juu ya sheria na wao kama Jeshi la Polisi watahakikisha wanawachukulia hatua wote wanaohusika kwani watakuwa wanavunja sheria ya nchi.

“Wambie tutawashughulikia kweli kweli … wanafanya vitendo hivyo sababu kuna amani na kama hakuna amani hakuna siasa na kama kuna mwanasiasa anasababisha vurugu huyo sio mwanasiasa,” alisema Kamanda Sirro.

Kamanda alieleza wazi kuwa askari aliowapeleka katika uachaguzi huo ni wachache na siku nyingine ataweka askari wengi zaidi ili kuwazuia wote ambao wanasababisha vurugu na tayari wamefungua jarada kwa ajili ya walio husika na kusababisha vurugu.

Pia Kamanda alizungumzia kitendo cha waandishi wa habari kuzuiliwa kuingia ndani ya chumba cha uchaguzi wakati uchaguzi huo ukiendelea na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi kama hicho na sababu ya kufanya hivyo ni kuweka usalama kwanza ili kuzuia vitendo vya vurugu.
 
Ok kamanda kwa hiyo uchaguzi ujao utaweka askari mia nane kwenye uchaguzi wa mayor na naibu mayor, wapiga kura hawazidi 200, wote wanasiasa na hakuna vijana wa Bodaboda, ili kuepusha hilo Masaburi aendelee kuwa Mayor wa jiji kuliko kuendelea kuvunja amani ya Dar kwa uroho wa madaraka
 
ccm bila polisi ni wepesi kuliko pamba , lakini mh kamanda anatakiwa afahamu kwamba kabla yake alikuwepo kova , ambaye hata mwezi haujaisha tangu astaafu lakini amekutwa mahakamani akigombea nyumba ya bure ! malipo ni hapahapa .
Kizuri ni kwamba ameshinda kesi
 
Kamanda Siro ukianza mambo ya kujipendekeza kwa CCM kazi itakushinda
Pitia mafaili uone majizi,wakwepa kodi,wezi wa EPA ESCROW na wauza unga ni wafadhili wa chama gani
 
Kama kamanda Simon Sirro hatambui hata chanzo za vurugu hizo anazodai aliwatuma vijana wake kwenda kudhibiti, basi ana matatizo na hafai kuwa "kamanda!"

Labda tumfahamishe kuwa, chanzo za vurugu hizo ni mbinu za wanasiasa walioko serikalini na wale wa CCM kuchelewesha uchaguzi wa umeya wa jiji la DSM bila sababu zozote za msingi!

Angeelekeza ushauri wake huko ili zoezi hilo lifanyike na wao kama polisi waendelee na majukumu yao mengine ya kawaida ya kila siku, angeeleweka vizuri zaidi.

Lakini kwa kauli hii, nathubutu kusema imekaa Kijecha jecha zaidi, yule bwana wa kibaraghashia aliyesababisha songombingo la Zanzibar!!

Yaani yeye kamanda anazungumzia hao anaowaita "wanasiasa", defenetely anawa refer wale wa vyama vilivyo nje ya serikali....kwake yeye hao ndio "wanasiasa!".

This is wrong target na lazima atashindwa tu na atai miss!!
 
Back
Top Bottom