tanganyika yetu
Member
- Nov 23, 2011
- 45
- 17
Awali ya yote nielezee aina ya watalii wanaokuja Tanzania, nchi yetu inapata au kupokea watalii aina nne:
1. Kuna watalii wa bajeti (budget), 2. Watalii wa Kati (mid class), 3.Watalii wa Juu (high class) na Watalii wa juu zaidi (High end).
Watalii wa bajeti na wakati ndo wengi ni kati ya 70% - 80% na wanaobaki ni watalii wa juu na juu zaidi, na ukitaka kulijua hili ni utafiti mdogo sana (hahitaji kuwa na digrii); kwa watalii wa low class na mid class; angalia low (budjet) class na mid class accommodations ziko ngapi; utakuta ziko nyingi sana na angalia camp site za basic camping ziko ngapi; utaona ziko nyingi, sasa tugeukie high class & high end accommodations; utakuta ni chache sana! Kama waziri anasema anahitaji watalii matajiri yaani high end ni kwamba hataki visa, park fee, camping fee ya watalii wa low class, mid class ama high class, kwa msingi huu serikali itakusanya tu visa, park fee na camp fee za watalii matajiri sana (high end). Nashindwa kuelewa kwanini Waziri hataki watalii ambao si matajiri ili hali visa, park fee na camping fee inalipwa sawa kwa Makundi yote yaani watalii wote wanalipa visa na park fee inayolingana, haimanishi akiwa top end analipa visa au park fee zaidi! Mimi ningemuelewa waziri kama angesema watalii matajiri (high end) walipe visa na park fee kubwa zaidi ya wengine.
KUPANDA KWA TOZO NGORONGORO: Mimi sina ubishi sana na ongezeko husika hususan entry fee lakini sikuona umuhimu wa kuongeza carter service fee. Sasa tatizo yangu kubwa ni taarifa ya muda mfupi mno! Haingii akilini taarifa ya tozo mpya inatolewa tarehe 25 Juni na inatakiwa ianze kutumika julai mosi, ni siku sita tu zimebaki tozo mpya ianze kutozwa! Hili linasikitisha sana; kwanini iwe gafla hivyo? Kwanini basi taarifa haikutolewa angalau miezi 2 au 3 nyuma? ikumbukwe kwamba mtalii anapopanga safari anakuwa ameshapanga bajeti sasa unavyomuongezea gharama analalamika na anakosa furaha na hamasa ya holiday yake yamkini anaanza kupata stress! Haiwezekani mwenye nyumba akampandishia mpangaji kodi ya mwezi ujao wakati imebaki siku sita, kwa kawaida na kistaarabu anatakiwa ampe mpangaji taarifa mapema si chini ya mwezi ili mpangaji ajiandae na ajipange. Kila kitu kina utaratibu na mipango hata Mungu wetu ni wa utaratibu na mpango, hivyo hili swala la ongezeko la tozo ngorongoro ni vyema likawekewa utaratibu mzuri.
TOZO LA ONGEZEKO LA DHAMANI KWENYE UTALII (VAT - 18%): Mimi nafikiri viongozi wetu hawajafanya utafiti mzuri au wakutosha na hili linatokana na kutoshirikisha wadau na kama wadau wanashirikishwa basi nikwamba yale wanayoshauri yanapuuzwa na yanadharauliwa. Kimsingi Tanzania imekuwa eneo ambalo ni ghali sana kusafiri au kuja kutalii ukilinganisha na nchi zingine nyingi za Africa hususan nchi za Africa Mashariki; na baaadhi ya maeneo ambayo yanafanya utalii kuwa juu ni flight tickets (Local & international flight fare), accommodations, park fee, camping fee n.k.
Hii hapa chini ni Kauli ya Waziri wa fedha:
Akizungumzia VAT katika utalii, Dk Mpango alisema kodi hiyo haihusiani na ongezeko au kupungua kwa watalii nchini kwa kuwa watalii hao hawatazami kodi hiyo kama kigezo kikuu cha kwenda kuangalia vivutio vya utalii.
Alitoa mfano wa idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama kwa kipindi 2011 hadi 2014 katika nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, ambayo inaonesha Tanzania licha ya kwamba haikuwa ikitoza VAT, bado ilitembelewa na watalii wachache kuliko nchi hizo ambazo zilikuwa zikitoza kodi.
Kama waziri anatuambia na anakiri kwamba Tanzania ilitembelewa na watalii wachache ukilinganisha na nchi ambazo zina VAT basi ni vizuri akatuambia ni sababu zipi zilifanya Tanzania ipate watalii wachache ili hali haina tozo ya ongezeko la dhamani na atuambie ni kitu gani sasa kitafanya mwaka huu (2016/2017) watalii waongezeke baada ya gharama kupanda kwa ongezeko la VAT. Pia atuambie ni kwanini hizo nchi zenye VAT zilipata na zinaendelea kupata watalii wengi kuliko nchi hii. Tanzania inapata watalii wachache si kwasababu haina VAT bali ni kwasababu gharama ziko juu na hili linazungumzwa na watalii wenyewe.
Hivyo kama kweli serikali inataka watalii waongezeke basi haina budi kupunguza tozo na kodi lukuki ambazo mwisho wa siku ana beba mtalii. Lakini endapo serikali itaendelea kulazimisha VAT basi itapata majawabu muda si mrefu. Nchi ambazo waziri ametolea mfano kuwa zina VAT kwenye utalii na na bado zinapata watalii wengi ni sawa kabisa LAKINI ni ukweli kwamba pamoja na hizo nchi kuweka VAT bado gharama (safari package) ziko chini ukilinganisha na Tanzania, na mfano mzuri ni nchi ya Kenya; kwa mfano; safari ya siku saba mbuga za Kenya iko chini kwa 10 -15% ukilinganisha na Tanzania. Na ijulikane kuwa wanyama na vivutio ambavyo viko kwetu na jirani zetu wanavyo pia na wanafanya jitiada kila kukicha ili wapate watalii wengi zaidi na ndo maana wenzetu wameondoa VAT kwenye utalii.
Leo niliwasiliana na mkenya mmoja kumwabarisha ongezeko la tozo ngorongoro na VAT kwenye utalii; jamaa alifurahi sana akasema sasa biashara ya utalii Kenya itakuwa nzuri kwani watalii waliyokuwa waje Tanzania watageukia Kenya! Na huu ndo ukweli wenyewe, sasa kama VAT itaendelea kuwepo kwenye Utalii basi Tanzania itaambulia tu wale wageni anaohitaji waziri wa utalii (Mh. Magembe) ambao ni matajiri (top end) na sioni wakizidi 15% ya watalii wote Tanzania.
Kwa mfano kama Tanzania inapata watalii 2,000,000 kwa mwaka basi itapata watalii 15% ambayo ni watalii 300,000 tu, kwa msingi huu kampuni za kitalii zaidi ya 50% zinazotegemea wageni ambao si matajiri zitakosa wageni hivyo zitakufa na zikifa serikali itakosa mapato makubwa (mfano mdogo tu ni leseni ya utalii ambao ni US$2000 kwa kila kampuni kwa mwaka), watu wengi watakosa ajira, wafanya biashara wengi watakosa biashara na wateja (mfano wauza mafuta ya magari, wauza spea, wauza vitu sokoni, wauza vifaa vya ujenzi na vitu madukani, wenye migahawa, wenye bar na wauza vinywaji vyote n.k) hoteli nyingi zinazotegemea watalii ambao si matajiri zitakosa wageni, Serikali itakosa mapato ya visa na park fee!! Kimsingi hili litaleta madhara makubwa na kwa wengi. Baada ya wageni /watalii wengi kusikia kutakuwapo na ongezeko la VAT wameanza ku- cancel safari!
NINAOMBA SANA SERIKALI KW AUJUMLA WAKE NI PAMOJA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA, WAZIRI WA FEDHA, WAZIRI MKUU, BUNGE NA MH. RAISI; WAANGALIE TENA VIZURI HILI SWALA LA VAT KWENYE BIASHARA YA UTALII.