Kama umepona hapa mshukuru Mungu

Kama umepona hapa mshukuru Mungu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
11,574
Reaction score
14,646
Ndugu zangu Watanzania poleni kwa matokeo mabaya jana dhidi ya Uganda, ndio mpira ulivyo, asiyekubali kushindwa si mshindani. Wale mlio katika funga Mungu awasaidie na azipokee funga zenu.

Kwenye maisha watu wanapitia vitu vingi sana iwe kwasababu ya hali ya kiuchumi au kwasababu ya mazingira au sababu nyingine zilizo nje ya uwezo wetu, ila kama umepona kwenye haya yafuatayo mshukuru Mungu na uende ukatoe sadaka unapo abudu.

1. Kupeti: Yaani kama haupo kwenye hii addiction shukuru Mungu, ni moja ya addiction mbaya sana. Ukiingia huko kutoka ni shida watu wengi wanapata tabu kutoka na kujaribu kuacha ila wameshindwa.

2. Ponografia: Sijafanya utafiti, ila 90% ya watu wamepitia kwenye hii addiction au wapo kwenye hii addiction na ndio maana kule USA ni moja kati ya industry inayoongoza kuingiza hela licha ya kila mtu kukataa kuangalia picha hizo. Katika addiction zote ukiingia humu hutoki usijaribu.

3. Pombe: Nakumbuka kuna kipindi nipo O'Level kuna mwanasheria mmoja alikuwa na cheo kikubwa tulienda kwake kwa ajili ya issue za familia, nilienda na my parents, tulivyomaliza kilichotupeleka aliwaambia wazazi wangu kama wanaweza kumsaidia baba yake kuacha pombe kwasababu ametumia kila njia ila hajafanikiwa, aana ilikuwa akilewa anapata tabu sana na anafanya vitu vya ajabu ukiingia humu hutoki.

4. Madawa ya kulevya: Jaribu vitu vyote unaweza ukaacha ila sio drugs, ile kitu haifai kabisa. Yaani ukiingia kutoka ni mpaka tunakuzika, kwasababu arosto yake ni mbaya sana. Ninae mtu wa karibu ambaye ameathrika vibaya sana na hii kitu, mifano ipo mingi mpaka kwa wasanii, Mungu atusaidie tu, ila hii ngoma nzito.

5. Wanawake wa kununua: Kuna jamaa yupo kwenye ndoa ila yeye kwenye suala la kununua wanawake na totoz ni kama hajaoa vile, haipiti siku bila kula mzigo kiufupi jamaa amekuwa addicted na hayo mambo hii kitu isikie unaweza sema mtu ana jini mahaba.

Mimi nilikuwa muhanga wa betting na pornography kipindi cha nyuma ila nilikuja kuacha. Baada ya kuibiwa simu yangu nikakaa mwaka bila simu, nilipokuja kupata simu nyingine nikapoteza kabisa interest na hayo mambo mpaka leo nimeacha, nipo sawa kabisa, namshukuru Mungu kwa kunivusha kwenye lile jinamizi.

Pornography and betting are destroying your life by suppressing your brain ability and depressing your mental power, lets quit in a peaceful manner and better a future, believe you can do it.

Welcome to share your experiences.
 
Utarud chamani ni suala la muda...

Chaputu vs betting welcome mwana mpotevu...........
 
Back
Top Bottom