BENETH MENGELE
Member
- Sep 16, 2017
- 20
- 8
Hivi sasa ile mizizi ya umoja ambayo Baba wa Taifa ali isimika inapotea, kwani kwa kiasi fulani imasababishwa na kule kujidai, kujua kwingi kwa mambo ambayo hayana tija kwa jamii yetu ya kitanzania.
Wasomi wengi ambao taifa kwa namna moja au nyingine walisomeshwa kwa kodi za wananchi lakini uwezo wa kufikiri ni mdogo sana, mtu huyu ni Waziri au mkuu wa wilaya au mkoa utamuonea huruma hawezi lakini amesoma hadi vyuo vya nje. Kama Taifa, naomba viongozi wachukue hatua kuanzia ngazi ya chini au kama familia kuokoa kizazi cha sasa ambacho uwezo wa kufikiri hamna lolote.
Vijana wa leo hataki kusoma hata kama atamaliza chuo kikuu, baada ya hapo hana tena muda wa kujisomea. Maktaba ya nyumbani hana au ajitume ktk utafiti hawezi, yaani uvivu wa kujisomea umemtawala. Ikumbukwe kuwa umaskini wa mawazo ni mbaya kuliko wa mali. Ushauri wangu kwa Watanzania na serikali ihamasishe vijana ,tuitumie mitandao kwa faida kujiendeleza kielimu badala ya kutumia lugha isiyo faa tena kutoka kijiweni.
Biblia inatuambia kwamba watu wangu wana angamizwa kwa kukosa maarifa. Tuna angamia kweli kwasababu tumedharau misingi ya Baba wa Taifa. Watanzania wenzangu tusome na tuiunge mkono serikali yetu ili mkakati wa kusogeza nchi mbele ufanikiwe.