Kama Simba mmemuacha Sadio Kanoute basi mjue mmeiua rasmi Simba Sports Club

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
439
1,756
Sadio Kanoute amebadilika sana, sasa hivi amezoea mazingira, namwelewa sana hasa kipindi hiki cha Benchika, lkn kuna tetesi kuwa ameachwa kumpisha Babacar Sarr, aisee kama ni kweli tumekwisha.

Leo nimeona katika mchezo dhidi ya Jamhuri amekosekana kabisa kiungo wa kupandisha timu mbele, na kwa vile hata benchi hakukaa leo ni dhahiri kabisa kuna uwezekano huyu raia wa Mali ametemwa.

Nisipomuona na Singida keshokutwa ndio nitaamini kabisa na ndio itakuwa mwisho wangu kuendelea kuwemo humu ktk Jamiiforums.
 
Huyo kanute anafanyaga nini cha maana zaidi ya kucheza rafu na kurusharusha mikono kwa waamuzi? Sadio na Saido ni mizigo mizito hapo Simba.
 
Kwa viongozi hawa wa Simba sitashangaa ikitokea wamefanya hivyo. Timu ina shida kubwa sana ya mshambuliaji wa kati wao kila siku wanasajili mawinga tokea dirisha kubwa lililopita. Hao mawinga sijui wanenda kumpigia nani krosi afunge maana Boko sasa hivi hata kutuliza mpira vizuri ameanza kushindwa umri unamtupa mkono na Baleke sijui kakumbwa na nini. Baleke nahisi anahitaji zaidi mtalaamu wa saikolojia tena haraka sana maana si kwa kukosa kule magoli ya wazi kabisa. Wakati Baleke alipokuja alidhihirisha kuwa ni mfungaji bora kabisa tena akifunga magoli magumu kabisa ambayo kwenye ligi yetu ilikuwa ni nadra sana kufungwa.

Kwa mtizamo wangu sasa hivi Simba baada ya kupata kiungo mkabaji inahitaji sana washambuliaji wawili wa kati kumpa changamoto Baleke mmoja awe mzawa na mwingine awe wa nje. Na viongozi wafanye maamuzi magumu ya kuachana na Saidoo na Boko wampe majukumu mengine kwenye benchi la ufundi. Ikitokea Boko bado anataka kucheza basi aruhusiwe aende kwenye timu nyingine huko akazurure akishachoka kabisa arudi Simba kwenye benchi la ufundi au majukumu mengine ndani ya klabu ya Simba.

Ni mtizamo tu
 
Uko sahihi
Ni muda wa saidoo kuondoka simba
 
Sisi hatupendi kuwatukana nyie wanasimba
Shida ni viazi kams hawa ndio sababu
 
Mashabiki wa Simba akili mmepeleka wapi? Simba inasadikika kumuacha Sadio, sasa JamiiForums inahusu nini hapo?
 
Sadio Kanoute amebadilika sana, sasa hivi amezoea mazingira, namwelewa sana hasa kipindi hiki cha Benchika, lkn kuna tetesi kuwa ameachwa kumpisha Babacar Sarr, aisee kama ni kweli tumekwisha.

Leo nimeona katika mchezo dhidi ya Jamhuri amekosekana kabisa kiungo wa kupandisha timu mbele, na kwa vile hata benchi hakukaa leo ni dhahiri kabisa kuna uwezekano huyu raia wa Mali ametemwa.

Nisipomuona na Singida keshokutwa ndio nitaamini kabisa na ndio itakuwa mwisho wangu kuendelea kuwemo humu ktk Jamiiforums.
Ingekua vizuri ungethibitisha habari kwanz ndipo uilete public,vinginevyo ni hisia zako tu
 
Back
Top Bottom