Kama polisi wameshindwa kukamata wauaji hawa basi watangaze kuwa wameshindwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama polisi wameshindwa kukamata wauaji hawa basi watangaze kuwa wameshindwa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Deofm, Apr 30, 2012.

 1. D

  Deofm JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waheshimiwa wana JF,
  Duniani kote haki ya mtu kuishi ni haki ya msingi na huwa inalindwa kwa garama yoyote ile, jukumu hilo kwa kawaida limekabidhiwa kwa jeshi la polisi na vyombo vingine vyote vya usalama. Bila kujali hadhi ya mtu aliyeuawa, polisi walitakiwa wawakamate wauji na kuwafikisha mahakani. Lakini cha kushangaza ni pale anapotokea raia na kuwahimiza polisi watekeleze wajibu wao lakini wanaanza kutishia kumkamata na kumfungulia mashataka ya uchochezi. Nadhani wakuu mnakumbuka ishu ya Slaa na RPC wa Mwanza.

  Kwa hii hali ya mauji kuendelea nchini kwanini waziri na wasaidizi wake katika Taasisi hii wasiwajibike??
   
Loading...