Kama mwanamke una tabia hizi utazeekea nyumbani

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,615
2,031
Kuolewa ni ndoto ya kila mwanamke aliyekamilika ila kama una tabia hizi utazeekea nyumbani

1: Tamaa ya utajili,fedha na mali pasipo kujua kuwa mali na vitu hutafutwa

Hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kuwakataa wanaume wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjini.

2: Dharau,Maringo na mashauzi Classic

Yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha unamsonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua labda umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana una nyodo nyingi.

3Huna juma pili wala Ijumaa yaani huwendi kanisani wala msikitini, Lazima wahuni watapata nafasi ya ya kukuchezea hadi pale utakapochoka

MUNGU NI NGUZO KUU YA BARAKA ZAKO ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomoni mwa dubu na fisi wanaokuvizia na kuja kama malaika. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa

Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti kavaa kama mcheza show za night club, yaani akipita nguo inaonesha kila kitu na akiinama ndio balaa kabisa yaani kimini kinafunua kila kitu nje nje. Kwa staili hiyo nani atakupeleka kwao?

5.Kujipaka mirangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kimakonde, au kizaramo eti wenyewe wanaiita make-up kwanza mnatutisha tu

6: Kupenda kujirahisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume, yaani ukiguswa kidogo tu twende...

7: kuwa na picha karibia 500 facebook,twitter na instagram halafu picha zenyewe hazieleweki yaani umepigws kayika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu,mara umebinua makalio,mara tumbo mara mdomo

8: kila unachokifanya basi unakimbilia kupost

Mfano kwenye Facebook yako au Instagram na nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

9: Ni mtu wa maneno maneno tu.

Yaani we kila unachokiona unakiongea na kuropokaropoka tu hauna breki, mwanamke gani?

10: Huna mawazo ya malengo endelevu

Yaani we kwenye bichwa lako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu kafanya nini? Sijui Kim, Rihanna, Adelle wamefanya vile na upuuzi mwingine.

11: Mizinga

Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza "Baby nataka Samsung Galaxy, mara iPhone 7, mara baby nimeona nguo nzuri, mara ooh! baby yaani njaa inauma……kwa hayo mtaishia kusindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama. Waswahili husema, "Kama mzuri, olewa" Jihadhari na tabia hizi.

Wanawake samahanini sana mtanisamehe sana napenda sana kuwarekebisha ili mwende sawa na wanaume tunavyohitaji tunawapenda sana tatizo mna tuwangusha nyiye wenyewe
 
Back
Top Bottom