Kama mbwai iwe mbwai, viongozi wa Simba vunjeni kibubu mchukueni Mayele na Diarra!

J93

Member
Jun 20, 2016
50
149
Ndio kwani shida ipo wapi bhana?

Kama hela kwenye kibubu hamna, semeni mashabiki na wanachama tutachanga kuhakikisha Simba inawafanyia umafia na kuivunja vunja yanga kipindi hiki!

Raha ya mashabiki wa simba ni kuona yanga(utopolo) ikisambaratika na kuibuka migogoro isiyotatulika!

Yanga kwa sasa ni kama wameshiba na kuvimbiwa ndio maana wanaweza kuingiza siasa zao na kutishia kuwachukua wachezaji wa simba na mashabiki wakapata sintofahamu!

Hivyo simba itumie njia zote za kimafia inazozijua kuhakikisha kwanza wanamchukua Mayele haraka iwezekanavyo na kisha golokipa wao Diarra!

Haiwezekani utopolo itawale kipuuzi puuzi wakati Simba ina viongozi hodari. weledi na majasusi wa mpira!!!
 
Back
Top Bottom