Kama makanisa yataendekeza kwaya kuimba style za Mayele kanisani mimi nitaacha kusali

Mimi huwa nakereka sana katikati ya ibada inasimama kwaya kuimba mwishoni wanaanza kucheza style ya Mayele kwa kupiga mikono na kutetema, hicho kitendo ni cha kipuuzi sana!

Kwanza mnajua huwa anamaanisha nini? Au kila mtu aje na style ya mchezaji anayempenda tucheze kanisani?

Tuheshimu ibada, mwambieni Mayele awakataze mashabiki zake kabla hakijamkuta cha kumkuta!
unamtishia nani nyau?
 
Kwani ukiacha hasara ya nani?
Hiyo ni mayeles effect
 
Duuuuuuu!!¡! Dini ya kikristu bwana inashangaza sana,akija mchezaji mwingne na style nyingne wataimba kwa style hiyo.Ndugu yangu zinduka hiyo sio dini ,hicho ni kikundi cha wauuni wanakutana na kuwashawishi watu wapeleke sadaka ili wakazipige.
Ila ukweli utabaki palepale kwamba dini haimwingizi mtu mbinguni sasa usifikiri ukisema hivyo basi kuna mbadala, hakuna.

Kuwatendea wenzako yale unayopenda utendewe na wewe ni tiketi tosha kabisa ya kukuingiza mbinguni hayo mengine ni siasa tu za duniani na watu kujitafutia ulaji na ujiko.
 
Wewe acha ushamba kama tayari pepo ameshakuvamia anataka kukuzuia usiende kanisani hiyo ni shauri yako.

Huo ushangiliaji wa Mayele mbona aliutoa kwenye kanisa la kwao Congo tena la kiprotestanti la jijini Kinshasa wakiimba kwaya na kucheza kama hivyo na ni kawaida kabisa kwa makanisa ya Congo watu kuimba kwaya na muziki kama Mfalme Daudi alivyomuimbia Mungu, 2 Samwel 22:1
 
Huu mnaoita "Ukristo" siyo Ukristo ni upagani ulioboreshwa. Kanisa lililoanzisha aina hii mpya ya "upagani" ni kanisa katoliki zaidi ya miaka 1900 iliyopita.

UKRISTO wa KWELI ni tofauti kabisa na ukristo mnaoujua sasa. Nitaorodhesha sifa za UKRISTO wa KWELI.
  • kuzishika kwa dhati Amri zote kumi za MUNGU bila kubadilisha hata moja.
  • kushika Imani ya YESU KRISTO pasipo kuyumba.
  • kujitenga na sanamu, misalaba, picha na kila aina ya upagani.
  • kukusanyika na kuabudu siku ya "saba" kama KRISTO alivyofanya na kama MUNGU alivyoagiza.
  • wanawake kukaa kimya kabisa wawapo kanisani kama BWANA alivyoagiza maana hawana ruhusa kunena wala kufundisha.

Hayo ni machache tu, lakini yapo mengi.

Ukweli ni kwamba kanisa lolote lile linaloabudu siku ya Jumapili, kanisa hilo siyo kanisa la KWELI la KIKRISTO!!

Msingi mkuu wa UKRISTO ni "torati" na "Injili" (Mathayo 5:17-19) (Ufunuo 14:12) (1 Wakorintho 7:19)
 
Mimi huwa nakereka sana katikati ya ibada inasimama kwaya kuimba mwishoni wanaanza kucheza style ya Mayele kwa kupiga mikono na kutetema, hicho kitendo ni cha kipuuzi sana!

Kwanza mnajua huwa anamaanisha nini? Au kila mtu aje na style ya mchezaji anayempenda tucheze kanisani?

Tuheshimu ibada, mwambieni Mayele awakataze mashabiki zake kabla hakijamkuta cha kumkuta!
Simple: ukiona kanisa la aina hiyo basi hao ni wajasiriamali na siyo kanisa. Siku hizi inabidi kuwa makini ili uweze kutofautisha kati ya kanisa na utapeli. Kwa taarifa yako matapeli wengi wamehamia nyumba za ibada kwani wanajua huko ndiko rahisi kutapeli.
 
Back
Top Bottom