Kama kweli Tunajiita Taifa lisilo na ukabila!! Kwanini Serikari bado inaendelea kukusanya takwimu kwa ukabila?

Mr Chromium

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
2,088
2,705
Naamini kwa hapa Africa mashariki sisi tunajipambanua kama Taifa ambalo limemaliza ukabila au halijagawanyika kimisingi ya ukabil.!Hasa ukilinganisha na nchi kama Kenya, na Rwanda au wengineo!! Tumeunganishwa na kiswahili
Lakini cha ajabu ukienda hospitali unavoandikishwa una ulizwa kabila lako!!

Ukilala lodge au gesti kwene daftar/kitabu cha wageni kuna sehemu ya kabila la mteja na unaulizwa!!

Naelewa kistatistic itakua na umuhimu fulani lakin sidhan kama inaumuhimu kuliko kuwaleta watanzania pamoja!!

Je, hakuna namna ya kukusanya hizo taarifa kwa namna nyingine? Kwann isifike mahali mtu akiulizwa aseme “mimi n mtanzania fullstop!”

Naombeni kujua!!
 
Polisi wana mtindo huu wa kuripoti uhalifu wanapozungumza na waandishi wa habari. Hata hivyo imetusaidia kutambua kwamba matapeli, waporaji, wanyang'anyi wa ardhi na majambazi wengi ni kabila Fulani linalopatikana mkoa mmoja Kaskazini mwa Tanzania.
 
Kuna asili ya makabila yana tabia za Uhalifu fulani,Magonjwa,Fulani na hulka fulani. Nikisikia Mkurya kaua Mtu kisa katukanwa sitoshangaa ila Mzaramo ni kitu ambacho sitegemei kuona anaua kisa katukanwa, Sitegemei kuona Busha pale Mbeya kwa Mnyakyusa ila Pale kwa Mdigo Tanga nitaliona tu lipo .Basi DNA na asili za maeneo bado zinatakiwa kujulikana ili kutatua baadhi ya magonjwa na Migogoro.
 
Hata wao (Serikali) hawajui ni kwa nini, wamerithi ktk Ukoloni kama mambo mengi tu bila ya kuhoji.
 
Nafikiri dhana ya kutokuwepo kwa ukabila Tanzania ni nadharia iliyopakwa mafuta yenye kuleta harufu nzuri na kuwa coated na rangi ya rubi ila kilichomo ndani tunaita “yaliyomo yamo”
 
Naamini kwa hapa Africa mashariki sisi tunajipambanua kama Taifa ambalo limemaliza ukabila au halijagawanyika kimisingi ya ukabila!Hasa ukilinganisha na nchi kama Kenya, na Rwanda au wengineo!! Tumeunganishwa na kiswahili
Lakini cha ajabu ukienda hospitali unavoandikishwa una ulizwa kabila lako!!

Ukilala lodge au gesti kwene daftar/kitabu cha wageni kuna sehemu ya kabila la mteja na unaulizwa!!

Naelewa kistatistic itakua na umuhimu fulani lakin sidhan kama inaumuhimu kuliko kuwaleta watanzania pamoja!!
Je hakuna namna ya kukusanya hizo taarifa kwa namna nyingine? Kwann isifike mahali mtu akiulizwa aseme “mimi n mtanzania fullstop!”

Naombeni kujua!!

Kujua kabila lako ni muhimu ili kujua hata asili ya sehemu uliko toka na hiyo haiondoi dhana ya kwamba Tanzania ni Taifa lisilo kuwa na ukabila Au udini. Watz Tuko fresh tu kutaja kabila sio issue labda kama wewe ni mhamiaji haramu, hapo itakuwa ngumu.
 
Msikiti unahusiana nini na kabila la mtu?

Ni bora ingekua wanaulizwa dini,hapo comment yako ingeleta maana,

Mleta mada analalamika ukabila kisha nawe inaleta udini! Inaonekana kuna dini inakutafuna sana nafsi yako sio?
Hivi,swali jepesi tu:Neno msikiti mna hati miliki nalo?Mkisikia msikiti tu mnaanza kuwaza yenu.Msikiti/sinagogi (ni neno lilelile kwa maana).Huku kijijini kwetu hakuna tofauti ya neno kanzu na gauni.Acha negativities,unakwama places!
 
Kuna baadhi ya magonjwa yanashambulia makabila fulani zaidi, takwimu za makabila ni muhimu kwa sekta ya Afya.
 
Kuna baadhi ya magonjwa yanashambulia makabila fulani zaidi, takwimu za makabila ni muhimu kwa sekta ya Afya.

Nakubali lakini hii hoja c msingi sana kama tunataka tuunde taifa moja lenye mgawanyiko
 
Back
Top Bottom