maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Tangu serikali ya awamu ya tano ianze mpango wa kubomoa nyumba za wananchi zilizojengwa mabondeni na sehemu zisizoruhusiwa ilinilazimu kuipitia kwa makini ilani ya uchaguzi ya CCM ili kuona jinsi utekelezaji wa jambo hili ulivyofafanuliwa.
Katika ilani hii ya uchaguzi ya CCM nimegundua kwamba suala la bomoa bomoa halimo na halikuwa kipaumbele cha chama hicho.
Katika pitia pitia yangu ya ilani za uchaguzi za vyama vya siasa vya nchi mbali mbali nimegundua kwamba ilani ya uchaguzi ndiyo mwongozo wa chama kinachoshika dola na wakati wote wa kampeni wagombea huhubiri na hutembea juu ya ilani za uchaguzi za vyama vyao.
Tukichukulia kwa mfano, wakati wa kampeni ya Rais Baraka Obama aliasisi na kuuingiza katika ilani ya uchaguzi wa chama cha Democrats, mpango uliojulikana kama Obama Care uliokuwa wa kutoa huduma bure ya afya kwa watu wa hali ya chini. Ingawa mpango huu haukuwapendeza sana matajiri wa Marekani kwa sababu ndio wachangiaji wakubwa wa mpango huo, Obama aliusimamia tangu wakati wa kampeni mpaka wakati wa kupitishwa kwake kwenye bunge.
Kwetu huku ni kinyume, Magufuli wakati wa kampeni yake hakusema chochote kuhusu bomoa bomoa aliyoianzisha ili wapiga kura wampime na wafanye maamuzi kutegemea na kauli zake. Wakati wa kampeni zake aliahidi mengine lakini sasa anafanya mengine ambayo hakuwahi kuahidi, inaudhi sana.
Katika hili nadhani hawatendei haki watanzania.