Kama kuna wakati wa kushangiliwa basi kuna wakati wa kuzomewa. Kama kuna wakati wakusifiwa basi kuna wakati wa kukosolewa. Kama kuna wakati wa kufurahiwa basi kuna wakati wa kuchukiwa. Kama kuna wakati wa kuungwa mkono pia kuna wakati wa kutoungwa mkono. kwa nini tunataka kuwalazimisha watu waishi kwa kanuni zinazohegemea upande mmoja tu wa kusifia, kushangilia na kuunga mkono tu? Je tumesahau kuwa Mungu ndiye aliziweka hizi kanuni ili mwanadamu awe mnyenyekevu na kumuheshimu Mungu aliyekamilika katika maeneo yote?
Achani kuwalazimisha watu kuishi nje ya kanuni alizotuwekea Muumba
Wanajigeuza ni miungu watu hapa duniani, wakitaka kusifiwa kwa nyimbo na mapambio.. Kisa wameshika dola, walinenalo wanaamini ndo amri, ukilipinga wanakupinda.. Wanadhani wataishi milele.. Maisha yanaenda mbele, wakumbuke haya..