Kama hupendi kukosolewa huna haki ya kusifiwa

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Maisha yote yamejaa kanuni. Tangu asili Mungu ameyawekea maisha ya mwanadamu kanuni. Hivyo tukiangalia kwenye Biblia katika kitabu cha Muhubiri 3:1-8

1Kila kitu kina majira yake,
kila jambo duniani lina wakati wake:
2Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa;
wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa;
3wakati wa kuua na wakati wa kuponya;
wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga;
4wakati wa kulia na wakati wa kucheka;
wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza;
5wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya mawe pamoja;
wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia;
6wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza;
wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa;
7wakati wa kurarua na wakati wa kushona;
wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea;
8wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia;
wakati wa vita na wakati wa amani.


Kama kuna wakati wa kushangiliwa basi kuna wakati wa kuzomewa. Kama kuna wakati wakusifiwa basi kuna wakati wa kukosolewa. Kama kuna wakati wa kufurahiwa basi kuna wakati wa kuchukiwa. Kama kuna wakati wa kuungwa mkono pia kuna wakati wa kutoungwa mkono. kwa nini tunataka kuwalazimisha watu waishi kwa kanuni zinazohegemea upande mmoja tu wa kusifia, kushangilia na kuunga mkono tu? Je tumesahau kuwa Mungu ndiye aliziweka hizi kanuni ili mwanadamu awe mnyenyekevu na kumuheshimu Mungu aliyekamilika katika maeneo yote?

Achani kuwalazimisha watu kuishi nje ya kanuni alizotuwekea Muumba
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,497
2,000
Wanajigeuza ni miungu watu hapa duniani, wakitaka kusifiwa kwa nyimbo na mapambio.. Kisa wameshika dola, walinenalo wanaamini ndo amri, ukilipinga wanakupinda.. Wanadhani wataishi milele.. Maisha yanaenda mbele, wakumbuke haya..
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
11,549
2,000
Anaetakiwa kusifiwa ni mmoja TU ndie Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, hakuna mwingi chini ya jua anaetakiwa kusifiwa bila kukosolewa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom