Kama Binadamu sasa tuache kutumia "Usafiri wa MAJINI" ndo maana ajali haziishi. Msafiri Asiwe KAFIRI tena

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Ni miaka mingi sana toka Mv Bukoba , Mv Spicies n.k hatukujifunza kitu. Bado ukikaa pale ferry ukaangalia vile vivuko vinavyojaza watu pasipo kipimo ndo utagundua nachozungumzia.

Nenda ziwa Victoria huko... n.k kama serikali itaamua kwa nia njema kuwa sasa kwenye Bahari na Maziwa itusafirishe kama binadamu ajali kama ya MV Bukoba na hii ya sasa ya MV Nyerere isingetokea.

Badala yake tumekuwa tukitumia usafiri wa "MAJINI" Majini yanaweza hata 1000 yakakaa kwa mtu mmoja. Hivyo pia kwa meli zetu hizi yangejaa sana na isizame.sababu majini hayachukui nafasi kwa maana ya uzito.

Serikali imekuwa haiwaoni wananchi wake kama ni Binadamu. Inawaona wao kama majini.umewahi panda mwendo kasi asubuhi na jioni ?ule si usafiri wa binadamu.kweli nakwambia utagundua nao ni usafiri wa "majini" binadamu hawashindiliwi namna ile kwenye Bus.

Serikali ni wakati wa kuanza kuwa ona wananchi hawa kama binadamu.karne hii MSAFIRI ASIWE KAFIRI tena. Maana hali ya kwenye vyombo vyetu vya usafiri ni ukafiri mkubwa sana unafanyika.wakati huo nyie mkitumia ndege na magari ya serikali yenye viyoyozi full time.
 
Back
Top Bottom