Kama angeshinda urais 2005 angekuwa rais wa maisha

Testar

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,604
12,808
Uraisi wake usingepita njia tofauti na ulikopita uenyekiti wa chama.

Katiba ingebadilishiwa gear angani ili kumruhusu kufanya ambayo angeyataka.

Bila shaka hadi leo angekuwa ndiye Rais kwa kuondoa ukomo wa madaraka.

Anachofanya kama mwenyekiti wa chama ndicho ambacho angekifanya kama angekuwa Rais wa nchi.

Pumzi ya kuongoza imemwishia lakini bado yupo tu.Kwa sasa hawezi kuongeza lolote jipya kwenye uongozi wake.Chini ya uongozi wake na kwa uoga wake chama hakiwezi kumpeleka mtu Ikulu kama Rais.

Hivi kweli kwenye umma wa watu zaidi ya 6M yeye ndiye mwenye sifa ya kuwa mwenyekiti tu?
Nahisi hata walio chini yake wanaogopa kumwita dikteta ingawa wanafikiri hivyo.

Tangu Doctor aondoke mambo yanakwenda mrama.Doctor aliyepo ana uwezo mdogo kuliko maradhi yanayokisumbua chama.

Tunamshukuru kwa jitihada, muda na nguvu zake binafsi alizoonesha kama mtumishi wa chama.
Kwa sasa inatosha......sasa ni wakati wa kupokeza kijiti kwa mwingine ili naye akimbize.
 
AF wana hubiri demokrasia
Kwani mbowe hakupigiwa kura?? Alishinda au aliiba kura?? Kwani fomu hazikuwa wazi kuchukuliwa?? Alikataza mtu kugombea uenyekiti yeye personally?? Mie nafkiri watakaoamua ni wanachama kma walimpa kura basi ataendelea wakimpa mwingine basi ataachia ila mpaka sasa hajavunja katiba yoyote ya chama wala kuuvurga uhaguzi wowote wa ndani na ndio maana bado chama hakijavurugika otherwise kuondoka kwa zitto au slaa ungekiuwa chama.

Ila demokrasia labda ungeongelea upande wa pili ambapo rais wao baada ya miaka mitano ya kwanza hawataki apingwe na yeyote na vile vile uenyekiti hauwezi kuombwa na mtu yeyote zaidi ya mtu mmoja tu sasa hapo nani anaminya demokrasia????

Mimi naamini mbowe angekuwa dikteta angelazimisha hata kugombea urais mara zote ila kudhihirsha hali sio hio ndio maana chadema haijawahi kurudia mgombea urais kila mtu alishiriki mara moja basi wala hakuwahi yeyote kung'ang'ania kugombea mfululizo sasa huo udikteta unatokea wapi????
Angekuwa dikteta angekubali slaa au lowassa agombee urais afu akishinda yeye mbowe awe chini yao ??? Dikteta huwa anakubali hilo??
 
unapokua Huna kitu ndiyo shida hata chai inaonekana bado hujapata.
 
Njaa zitawaua nyie vijana wa kijani, yaani asbh tu unaanza na utumbo kupost! Au unataka uwahi kwenye dirisha lenu la buku saba?!
 
Mwanasiasa ni mwanasiasa,

15936430_791712637659960_8757832561404617070_o.jpg
 
Ndiyo tatizo lenu kubwa huwa hampendi kuambiwa ukweli, hasa anapokosolewa dikteta wenu.
Hamna aliyekataa kukosolewa ila mkija na hoja zenye mantiki... sasa mleta hoja anasema mbowe angeng'ang'ania urais lakini cha kushangaza hata nafasi ya ugombea urais hajawahi kugombea zaidi ya mara moja sasa kma kweli ana uchu wa madaraka na huo urais wa Tanzania kweli angeacha kugombea urais 2010 na 2015??? Unajua njooni na sababu nzito sio hizi nyepesi nyepesi za kuokoteza.

Pia kuhusu uenyekiti ni kwamba katiba haikukufuta kikomo cha uenyekiti ila katiba ilipofanyiwa mabadiliko maoni ya wanachama hayakurudisha tena ukomo wa mwenyekiti sasa kilifutwaje wakati mabadiliko yalifanywa na yakaletwa mapendekezo mapya ambapo yalikuwa hayana kipengele hicho tena na chama kizima na wote walikubaliana nalo na ndio wakaipitisha katiba mpya kwa kishindo sasa mbowe analaumiwaje hapo??
 
Njaa zitawaua nyie vijana wa kijani, yaani asbh tu unaanza na utumbo kupost! Au unataka uwahi kwenye dirisha lenu la buku saba?!
Ila nani aliyekwambia kila anayempinga mtukufu wenu ni kijani?.........mimi nimetoa mawazo yangu, si muhimu yaheshimiwe ila negative assumptions hazitakiwi.
 
Kwani mbowe hakupigiwa kura?? Alishinda au aliiba kura?? Kwani fomu hazikuwa wazi kuchukuliwa?? Alikataza mtu kugombea uenyekiti yeye personally?? Mie nafkiri watakaoamua ni wanachama kma walimpa kura basi ataendelea wakimpa mwingine basi ataachia ila mpaka sasa hajavunja katiba yoyote ya chama wala kuuvurga uhaguzi wowote wa ndani na ndio maana bado chama hakijavurugika otherwise kuondoka kwa zitto au slaa ungekiuwa chama.

Ila demokrasia labda ungeongelea upande wa pili ambapo rais wao baada ya miaka mitano ya kwanza hawataki apingwe na yeyote na vile vile uenyekiti hauwezi kuombwa na mtu yeyote zaidi ya mtu mmoja tu sasa hapo nani anaminya demokrasia????

Mimi naamini mbowe angekuwa dikteta angelazimisha hata kugombea urais mara zote ila kudhihirsha hali sio hio ndio maana chadema haijawahi kurudia mgombea urais kila mtu alishiriki mara moja basi wala hakuwahi yeyote kung'ang'ania kugombea mfululizo sasa huo udikteta unatokea wapi????
Angekuwa dikteta angekubali slaa au lowassa agombee urais afu akishinda yeye mbowe awe chini yao ??? Dikteta huwa anakubali hilo??
hivi akili zenu huwa mnaziweka wapi??nyie nyumbu,demokrasia mnayo ihubili chadema ni ipi ,hiyo ya kumteuwa lowasa kuwa candiadate wa uchanguzi,kwa maamuzi ya mtu mmoja ????acheni ubwege chadema na ccm ni watoto wa baba mmoja tofati yenu mavazi tu ,chadema wanatafuta sehemu ya kupiga dili ,ccm tayari wamepata ,pambafu kabisa ,hizi porojo za demokrasia mwache kabisa ,kwani it is too fallacy ....
 
Kwani mbowe hakupigiwa kura?? Alishinda au aliiba kura?? Kwani fomu hazikuwa wazi kuchukuliwa?? Alikataza mtu kugombea uenyekiti yeye personally?? Mie nafkiri watakaoamua ni wanachama kma walimpa kura basi ataendelea wakimpa mwingine basi ataachia ila mpaka sasa hajavunja katiba yoyote ya chama wala kuuvurga uhaguzi wowote wa ndani na ndio maana bado chama hakijavurugika otherwise kuondoka kwa zitto au slaa ungekiuwa chama.

Ila demokrasia labda ungeongelea upande wa pili ambapo rais wao baada ya miaka mitano ya kwanza hawataki apingwe na yeyote na vile vile uenyekiti hauwezi kuombwa na mtu yeyote zaidi ya mtu mmoja tu sasa hapo nani anaminya demokrasia????

Mimi naamini mbowe angekuwa dikteta angelazimisha hata kugombea urais mara zote ila kudhihirsha hali sio hio ndio maana chadema haijawahi kurudia mgombea urais kila mtu alishiriki mara moja basi wala hakuwahi yeyote kung'ang'ania kugombea mfululizo sasa huo udikteta unatokea wapi????
Angekuwa dikteta angekubali slaa au lowassa agombee urais afu akishinda yeye mbowe awe chini yao ??? Dikteta huwa anakubali hilo??
Kama chama hakiruhusu mgombea kurudia zaidi ya mara mbili, yule aliyekwisha kujitangazia ugombea 2020 itakuwaje?
 
Hamna aliyekataa kukosolewa ila mkija na hoja zenye mantiki... sasa mleta hoja anasema mbowe angeng'ang'ania urais lakini cha kushangaza hata nafasi ya ugombea urais hajawahi kugombea zaidi ya mara moja sasa kma kweli ana uchu wa madaraka na huo urais wa Tanzania kweli angeacha kugombea urais 2010 na 2015??? Unajua njooni na sababu nzito sio hizi nyepesi nyepesi za kuokoteza.

Pia kuhusu uenyekiti ni kwamba katiba haikukufuta kikomo cha uenyekiti ila katiba ilipofanyiwa mabadiliko maoni ya wanachama hayakurudisha tena ukomo wa mwenyekiti sasa kilifutwaje wakati mabadiliko yalifanywa na yakaletwa mapendekezo mapya ambapo yalikuwa hayana kipengele hicho tena na chama kizima na wote walikubaliana nalo na ndio wakaipitisha katiba mpya kwa kishindo sasa mbowe analaumiwaje hapo??
Agombee urais wakati anajua hatashinda, urais akose ubunge akose marupurupu na mishahara aikose? ?
Unachekesha, unadhani kwanini Dr. Slaa alipogombea urais aliweka masharti ya kulipwa mshahara wa katibu mkuu na mshahara na marupurupu yote kama mbunge? ?
 
Hata wewe sijui unachangia nini.....r u sure lipumba anajua kuwa angeshinda urais 2000,2005,2010???? Ila mbona aligombea mara zote hizo??? Mrema je???

Hoja hapa sio pesa kma ni pesa mbowe anauwezo wa kuearn pesa zaidi ya hizo za ubunge nje ya siasa na wwe unalijua hilo maana hta hujui kuwa mzee wake mbowe alitoa hela ya nauli nyerere aende UN then unafkiri ana njaa kma wwe... so low.

Hoja hapa ni udikteta wa mbowe sio pesa... hivi dikteta huwa wanataka hela au nguvu?? Hitler alitaka pesa???putin??musolin?? Magufuli anakula hela kma kikwete ila je sio dikteta??? Nyerere kimataifa anahesabiwa kma dikteta je amewahi kula pesa???

Mleta mada anasema mbowe ana uroho wa madaraka sio pesa sasa huyo mroho gani wa madaraka ya urais akatae kugombea urais inaingia akilini kweli?? Ingekuwa lipumba ningekuelewa au mrema maana wamekuwa wenyeviti na pia wagombea urais muda mrefu sasa mbowe vp?? Kahodhi hizo nafasi?? Rais na mwneyekiti wa chama nani yuko juu kwenye maamuzi ya nchi hii??? Sasa angeshinda lowassa ina maana mbowe angekuwa chini ya lowassa kinguvu na ushawishi sasa dikteta huwa anakubali hili la kuzidiwa nguvu na mtu mwingine au kuwa chini ya mtu mwingine??

Acheni ushabiki vijana... mbowe kafanya kazi yake hata mkimtukana ila ndio kachangia sana kuifikisha chadema hapa ilipofika so mkimkejeli haijengi muhim na nyie jitahidini ili chama chenu kiongeze kura maana mbowe kajitahidi sana kuongeza kura kila uchaguzi nyie vp mbona zinapungua kwa kasi kila uchaguzi toka mbowe awe mwenyekiti???
 
Kama chama hakiruhusu mgombea kurudia zaidi ya mara mbili, yule aliyekwisha kujitangazia ugombea 2020 itakuwaje?
Huo nilitolea mfano tu ili kuonyesha viongozi wa chadema sio madikteta kma mnavyotaka kutuaminisha maana madikteta kweli wangekubali kweli kuachiana nafasi ya urais??

Anyway back to topic
We hoja yako si mbowe kuwa dikteta?? Anzisha uzi wa lowassa kuwa dikteta ntakujibu huko ila hapa usinihamishe mada maana najua kila mjadala siku hzi mpaka lowassa atajwe ndo mnaridhika.

Hiyo ya mgombea urais mnashikilia bango kila siku 2010 mlisema mbowe ghafla slaa..... 2015 mkasema slaa ghafla lowassa..... haya 2020 lowassa but anything can happen na mkashangaa mmeletewa kete nyingine hku nyie mshajipanga kukutana na lowassa......time will tell.
 
Ukiambiwa useme ni wapi nimemtaja Mbowe kama dikteta utaweza?
 
Back
Top Bottom