Kalapina wa harakati apewe support na rais,Dr JPM!

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Amani na iwe kwenu wana JF!

Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia harakati za msanii kalapina kwenye kupinga matumizi ya mihadarati au dawa za kulevya kupitia nyimbo zake na kipindi chake cha harakati kinachorushwa na clouds tv..

Kwa hakika utaungana na mimi kuwa jamaa ana juhudi kubwa na mpaka sasa ameshasidia vijana wengi!Hata hivyo naona jukumu la kupambana na dawa za kulevya halijatiliwa sana mkazo na serikali ya Dr. JPM (sina uhakika) hasa kwenye eneo la kushirikisha jamii zaidi ya kutumia police pekee kwa kiasi kikubwa.

Ndugu zangu hali ya matumizi ya mihadarati au madawa kwa vijana ni serious issue..mtaani kwetu kuna vijana napishana nao hali zao zinasikitisha au kukatisha tamaa..lakini kinachoniuma zaidi,jamaa wanaouza au kufanya hizo biashara naona serikali haijakomaa vya kutosha..

Ni wakati sasa wa serikali kushirikiana na wadau kama kalapina ambaye ameonyesha njia ya dhati kabisa ya kusaidia..Na kikubwa zaidi jamaa kwenye interview yake ya hivi karibuni na millard ayo, ameonyesha kujua mambo mengi sana na utayari wa kusaidia vijana zaidi!Inawezekana pia hata akasaidia kuwapata mazungu wa hii biashara.

Serikali impe support kubwa hasa ya kipesa au utaalamu/elimu zaidi huyu jamaa kama njia ya kuunga mkono juhudi zake..

Hebu angalia video alipokuwa akihojiwa na utakualiana na mimi kuwa jamaa yuko vizuri

Kalapina anafahamu vingi kuhusu Matibabu ya Chid Benz, kayaongea haya...(+Video) - TZA_MillardAyo

Ni maoni tu
 
Back
Top Bottom