Hakika unabii huo wa Askofu Kakobe unaanza kutimia kwa usahihi mkubwa sana.
Tumeyaona mafarakano hayo makubwa yaliyotokea kwenye chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wao wa Urais, hadi kusababisha mgombea mmojawapo EL kuachana na chama hicho alichokitumikia kwa miaka 38 na kujiunga na Chadema na leo kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chadema na Ukawa kuwa mgombea pekee kwa nafasi hiyo ya Urais.
Hakika kwa mwenendo huo wa mambo ya kisiasa na mafarakano makubwa yanayoendelea kwenye chama tawala ambayo yamesababisha chama hicho kikongwe kumeguka vipande vipande na kuwafanya makada wengi wa chama hicho kikongwe kujitokeza hadharani na kutangaza kuachana na chama hicho kikongwe na kujiunga na chama cha Chadema.
Ni hakika kuwa Mungu anadhihirisha ukuu na utukufu wake kutimiza hayo mapigo yake kwa chama tawala kutokana na chama hicho kuwapuuza wananchi wanaowaongoza badala yake watawala wetu wamekuwa na kiburi na kuamua kujitajirisha na rasilimali za nchi hii ambazo Mungu alizijaalia kwa Taifa hili kwa manufaa ya wanabchi wote wa Taifa hili.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.