chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,400
- 24,984
Habari wanaMMU.
Nina uhitaji wa ushauri kwa ajili ya ndugu yangu ambaye amejiingiza kwenye mtego ambao sasa ameshindwa kuutegua.
Naomba nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye kisa chenyewe kilichomsibu.
Ni kwamba huyu rafiki yangu wa karibu sana ambaye tumefahamiana tukiwa O level mpaka chuo amekuwa akinishirikisha masuala mbalimbali ambayo aliamini ninaweza kumshauri au kumtatulia ila kwa hili la leo naona limenizidi nguvu na nimelileta kwengu makungwi ili muweze kumsaidia huyu rafiki yangu kwani kila chochote mtakachoshauri nitampatia asome mwenyewe.
Kisa chenyewe:
NI KWAMBA ALIJIINGIZA KATIKA MAHUSIANO NA MKE WA MTU YAPATA MIAKA MITATU SASA, JAPO WANAISHI MIKOA MIWILI TOFAUTI NA HAWAJAWAHI KUONANA HATA SIKU MOJA TOFAUTI NA KUWASILIANA KWA SIMU WHATSAPP, FACEBOOK N. K
ANASEMA MWANAMKE HUYO AMEKUWA AKIMSAIDIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI HASA YA KIUCHUMI KWANI ANAKIRI MWENYEWE KWAMBA HAJAWAHI KULALA NJAA TOKA AFAHAMIANE NA MWANAMKE HUYO MTANDAONI.
PESA ZA KUBADILI MAVAZI NA VYAKULA HAVIKUWA ISHU SANA KWAKE KWANI MWANAMKE ALIGHARAMIA KILA KITU.
MPAKA KAFIKIA HATUA YA KUNISHIRIKISHA HAYA NI KWAMBA AMEONA ATAKUJA KUINGIA MATATANI BAADAE KWANI AMEMPATA MWANAMKE ANAYEMPENDA NA ANGETAMANI AWE MWENZI WAKE WA MAISHA, YAANI WAFUNGE NDOA NA KISHA WAANZISHE FAMILIA AWEZE KUACHANA NA HUYU MKE WA MTU AMBAYE ANAHOFIA YANAWEZA KUMKUTA MABAYA JAPO BADO ANATAMANI PESA ZA HUYU MKE WA MTU AMBAYE MAISHA YAKE SIYO MABAYA KWANI ANA NYUMBA YAKE KAJENGA MWENYEWE, KAZI NZURI NA USAFIRI AMBAPO HUYU MWANAMKE KATUMIA MALI HIZI KUMSHAWISHI RAFIKI YANGU KWAMBA BAADAE WATAKUJA KUISHI PAMOJA NA ATAMPATIA KILA ATAKACHOHITAJI HIVYO ASIHANGAIKE NA WASICHANA WASIOKUWA NA KITU NA MAGOLI KIPA.
KWA UTANGULIZI HUO HUYU JAMAA YUPO NJIANI PANDA NA ANAHOFIA ATAKAPOACHANA NA HUYU MKE WA MTU ANAWEZA KUMLIPIZA KISASI AU KUMPANGIA TUKIO LOLOTE LINALOWEZA KUHATARISHA MAISHA YAKE ENDAPO ATAKIUKA MATAKWA YA MKE HUYO WA MTU.
NDUGU YETU ANAHITAJI USHAURI WENU WADAU.
Chochote mtakachoshauri hapa nitampatia akisome mwenyewe.
Matusi na lugha zisizokuwa na staha hazifai, kama hutokuwa na la kumshauri unaweza kupisha wengine.
Karibuni tumshauri mwenzetu.