Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,513
- 10,666
Nimeandika uzi huu kichokozi ili wadau wakosoe pale nitakapokosea kwani nimetumia taarifa za zamani sana. Jina la Kaizirege lina asili ya Bukoba na nilposikia jina la shule mara moja nilidhani kama kawaida ya jamaa wa huko basi hii shule itakuwa inamilikiwa na Profesa ama Dokta flani, matokeo ya goole yalikuja tofauti kumbe ni KEMEBOS, hilo ndilo jina maarufu kwa wenyeji wa huko. Na ndio katika kuvuta kumbukumbu kumbe hata mmiliki wa shule hizi namfahamu na elimu yake ni ya kawaida, nadhani ni darasa la saba jamaa anaitwa Yusto Ntagalinda (nipo tayari kukosolewa)
Binafsi nilimfahamu mmiliki wa shule hii kwenye miaka ya 1990, wakati huo akiwa dereva na mmiliki wa mabasi ya abiria yaliyokuwa yakifanya safari za Bukoba to Izimbya maarufu kama Mukiza Bus Service, miaka ya 90 mpaka 93 niliishi mitaa ya Hamugembe jirani kabisa na huyu jamaa na hapo ndipo nilpomfahamu zaidi, huyu ni miongoni mwa watu wachache wachapa kazi niliowahi kuwafahamu...jamaa alikuwa dereva wa gari zake, huku yeye akiwa fundi makenika na kuna siku nilishuhudia saa moja jioni baada ya yeye kurudi trip ya Izimbya ambapo kuna moja ya vipuri vya gari zake kiliaribika na kuamua kuendesha gari dogo hadi Kampala kufuata spea ambayo ilifungwa usiku huohuo ili kesho gari liende Izimbya, barabara ya BkB - Kampala wakati huo ilikuwa ni mashimo na vumbi.
Baadae nilikuja kuambiwa biashara za usafirishaji pamoja na gereji aliacha na kuamua kuwa mvuvi wa sangara ziwa victoria, na ni kutokana na biashara za uvuvi aliweza kuwekeza katika elimu.....kwa waliowahi kuishi BKB mjini kule siasa za maji taka ndio kitovu chake ila nasikia jamaa yeye na siasa hawapatani, ukijifanya mwanasiasa kwake kazi huna.
Siri ya mafanikio ya huyu jamaa ni uchapa kazi, nasikia pia alikimbiwa na mke wake wa kwanza kwasababu ya jamaa kulala gereji! Wadau wa JF hasa wale waliopo Bkb maeneo ya Kabare wanayo mengi kuhusu jamaa huyu Yusto Ntagalinda.....