Kaitaba, Kagera: Kagera Sugar 1 -2 Yanga Afrika

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,514
2,730
Leo kutakuwa na mtanange wa kukata nashoka kwenye moja ya viwanja bora kabisa nchini, uwanja wa kaitaba huko bukoba, yanga atakuwa akitafuta points tatu muhimu ili kujikita kileleni mwa ligi na kuzidisha gap lake dhidi ya mtani wao, huku kagera sukari nao wakihitaji alama tatu muhimu kwasababu tangu kuanza msimu huu hawajawa na matokeo mazuri sana.

Kikosi cha yanga kina mabadiliko makubwa.... Walioanza ni Kabwili, Godfrey, Mwinyi Haji, Abdallah Shaibu, Vicent Chikupe, Feitoto, Ngassa, Maka Edward, Mateo Anthony, Jafari Mohamed na Makambo.

Update

Dakika ya 11 ya mchezo kagera 0 yanga 0.

Update

Dakika ya 20 ya mchezo gooooooooooool
Haritier Makambo anaiandikia yanga goli la kuongoza kwa njia ya kichwa.

Update

Kagera sugar wanapata mkwaju wa penalt hapa.

Anakwenda kupiga penalty Ramadhan Kapera gooooooooo kagera sukari wanarejea mchezoni katika dakika ya 32 ya mchezo.

Wakati huo huo kagera sukari wanafanya mabadiliko hapa, katoka Juma Nyosso kaingia Juma Shumvuni.

Update

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hapa uwanja wa kaitaba, kagera 1 yanga 1.

Kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza tunashuhudia kadi mbili za njano kwa wachezaji Ramadhan kapera wa kagera sugar na Paul Godfrey wa yanga.

Update
Dakika 45 za kipindi cha pili zinaanza hapa.

Update
Yanga wanafanya mabadiliko hapa, Heritier Makambo anakwenda bench na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajibu Migomba.

Feitoto nae anaonyeshwa kadi ya njano hapa baada ya kumchezea ndivyo sivyo Peter Mwalyanzi wa kagera sukari.

Update
Mwinyi Haji Ngwali beki wa kushoto anakwenda bench na nafasi yake inachukuliwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke.

update
70' kagera 1 yanga 1

Update
yanga anaandika goli la pili hapa,ni Raphael Daudi Lotti.

update
kagera sugar wanafanya mabadiliko hapa ,peter mwalyanzi anakwenda bench na nafasi yake inachukuliwa na Paul Ngayoma .

update
3+ zimeongezwa kabla ya kutamatisha mtanange huu.

Update

Mpira umekwisha hapa kaitaba kwa yanga kujichukulia alama zote tatu.

FT kagera sukari 1 yanga 2.
 
Back
Top Bottom