Kaimu Mkurugenzi wa jiji aahirisha uchaguzi wa Meya jiji la Dar es Salaam

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Uchaguzi Meya.jpg


Mzozo umezuka baada ya kaimu mkurugenzi wa jiji kuahirisha uchaguzi kutokana na watu ambao hawajawekwa wazi kufungua kesi mahakamani ya kuzuia uchaguzi huo huku wapiga kura wa CCM wakisusia na kuondoka.

Uchaguzi umeahirishwa hadi hapo utapotangazwa tena.
================

UPDATE

VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani.

Jambo hilo liliwachukiza madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia.

Wakati UKAWA wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo wenyewe ,Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini,jambo lilowachukiza tena na kuibua patashika ndani ya ukumbi.
 
Katika hali ya kushangaza uchaguzi wa Meya wa jiji la dar umehairishwa tena bila sababu za msingi,Hii tunaweza kuiita Ni demokrasia ya kijambazi,
Ccm wameikamata nchi nzima,Leo jiji tu wanashindwa kuliachia ingali wamezidiwa kwa number.Swala kama hili litatoa picha halisi kule zanzibar.
Kwa chama kikongwe kama Ccm hii ni aibu ya karne kwao.
 
Kama anayo Mamlaka kisheria ya kuahirisha na anazo sababu za msingi I see no problem!
 
Mzozo umezuka baada ya kaimu mkurugenzi wa jiji kuahirisha uchaguzi bila sababu za msingi huku wapiga kura wa CCM wakisusia na kuondoka.

View attachment 325985
Ebu tuambie kwanza sababu za kuahirisha na sisi tupime kama ni za msingi au sio za msingi maana umeleta uzi kibavicha bavicha hivi, kukuamini ni ngumu kuwa hakukuwa na sababu za msingi.
 
Hii sasa too much,,ccm inajitia aibu,,Kama kwenye umeya tu ivyo,ivi itaweza siku kuachia madaraka ya nchi ikishindwa,,,?;!!,,,MAGUFURI AINGILIE KATI ILI SUALA LA UCHAGUZI WA MEY WA JIJI AISEE,,,,,,
 
afu tunaambiwa hii serikali ya sasa ni ya haki! wizi mtupu. kila siku 'watanzania niombeeni' sasa kwa style hii si nikutochosha bure, make muombewaji naye kila siku anafanya madhambi sasa unategemea MUNGU atayafanyiaje kazi haya maombi yetu!
nami nasema watanzania hata tusimuombee tunapoteza nguvu za bure
 
Back
Top Bottom