Kagasheki asema, ‘Things are rotten’!

Kagasheki asema, ‘Things are rotten’!

asha ngedere

Member
Joined
Nov 6, 2009
Posts
92
Reaction score
12
Nimeipata sasa hivi hii wadau, naomba tuijadili...

Na Daniel Mbega, Iringa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Sued Kagasheki, amepuliza kipenga. Kilichobaki sasa ni kwa wachezaji kushiriki kikamilifu kupambana na ujangili, kwani mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wahariri wa habari nchini iliyofanyika leo mjini Iringa, Balozi Kagasheki amesema wimbi la ujangili linazidi kuongezeka kila kukicha kiasi cha kutishia uwepo wa Tembo pamoja na viumbe wengine, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kikamilifu mapambano hayo.

"Things are rotten and should be cleaned up (mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa)," amesema Waziri Kagasheki. "Ninyi waandishi ni wachezaji katika vita hii, ingawa mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye wajibu mkubwa wa kupambana na janga hili. Mchango wa wanahabari ni muhimu sana."

Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Balozi Kagasheki amesema, vita dhidi ya ujangili haiwezi kuonewa haya na akatoa rai kwa wanahabari kutumia taalamu yao kufichua maovu yote yanayohusiana na ujangili na kuutokomeza, vinginevyo vizazi vijavyo vitawahukumu.

Amesema vyombo vya habari visisite kuwafichua wahusika, hata kama waziri mwenyewe yumo kwenye mtandao huo, kwani maslahi ya taifa ni ya kupewa kipaumbele.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo, Balozi Kagasheki amesema haiyumkini kwa pembe za ndovu kukamatwa ng'ambo wakati makontena hayo yanajazwa na kusafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, hali ambayo inaleta taswira kwamba hata watumishi wa umma wanahusika kwa kiasi kikubwa.

"Pale bandarini kuna polisi, kuna customs (forodha), kuna TPA wenyewe, na kuna maofisa wa usalama. Inakuwaje basi meno haya ya tembo yanapakiwa pale na kusafirishwa, halafu yanakwenda kukamatwa Hong Kong, au Philippines, au Vietnam. Hapa kuna tatizo, lazima tuliseme," amesema.

Amesema rushwa kwa watumishi wa umma na waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hizo ni kubwa, hali inayoifanya vita hiyo kuwa ngumu.

Hata hivyo, amesema kuongezeka kwa ujangili kunachangiwa na mambo mengi, yakiwemo mahitaji ya meno ya tembo ulimwenguni, faida itokanayo na biashara hiyo kuwa kubwa, umaskini wa wananchi, na mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa umma.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, amesema pamoja na vita hiyo kuwa ya muda mrefu, lakini inakuwa vigumu kwa vile wahusika ni watu wenye fedha na hawaogopi kupoteza chochote.

Amesema wanahabari wanatakiwa kutokuwa waoga hata kama wanaopambana nao ni watu wenye fedha."Msiogope hata kama hawa wana mapesa, vita hii ni kubwa na tunapaswa kupiganwa kwa nguvu zote kuhakikisha tunatetea maliasili ya taifa," amesema.

Hata hivyo, amepinga takwimu za TAWIRI kuhusu idadi ya tembo wanaouawa kila siku na kusema mara nyingi takwimu hizo zinatengenezwa na maofisa kuilinda serikali huku katika uhalisi tatizo hilo likionekana kuwa kubwa zaidi.

"Hizi takwimu siyo sahihi na zaidi zimejikita kwenye maeneo yale tu yaliyo chini ya hifadhi, vipi kuhusu maeneo mengine ambayo hayatambuliki? Kwa hiyo, idadi ya tembo wanaouawa kila siku inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko tunavyoelezwa," amesema.

Lembeli amesema Idara ya Maliasili haina watumishi wa kutosha, bajeti ni ndogo na maslahi ni duni, hivyo kuitaka serikali, kama kweli imedhamiria kukabiliana na tatizo hilo, basi iongeze watumishi na kuwamotisha.

Amewataka wahariri hao wa habari kuunda Jukwaa la Marafiki wa Big Five (Friends of the Big Five) litakalowashirikisha wadau mbalimbali kuanzisha mijadala ya namna ya kupambana na ujangili pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, ameitaka serikali kuongeza kasma kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kama ilivyofanya katika sekta ya madini miaka kadhaa iliyopita.

"Sekta ya madini ilitengewa fedha nyingi zaidi, lakini hivi sasa wametuachia mashimo. Sasa ni wakati wa serikali kuitengea fedha nyingi idara ya utalii na maliasili kwa sababu kuna uhakika wa kuongezeka maradufu kwa pato la taifa kutoka asilimia 17 ya sasa," alisema.

Daniel Mbega ni Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la DARAJA LETU, ambalo ni la Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
 
Si walishaambiwa JANGILI MKUU ni nani na kuishia kumtetea pale Bungeni? Tena JANGILI lenyewe linaua Tembo na kusafirisha lenyewe! Sasa anacho taka wananchi wafanye ni nini?

Amesha kiri kwamba pamoja na taarifa mwisho wa siku serikali ndiyo inachukuwa hatua. awaambie waTnaganyika ni hatua gani wamezichukuwa kulishughulikia hilo JANGILI?

Vinginevyo wakubali tu kwamba MAGAMBA ni wabia kwenye hiyo biashara.

MSHIKWA NA NGOZI NDIYE MUIBA NG'OMBE.
 
hata kama wana pesa aziwezi kupambana na serikali kama itaamu....lakin serikali ikiwa dhaifu na anaye iongoza ni dhaifu ndo matokeo yake wenye pesa kuiamlia serikali katika utendaji wake
 
Kinana ndiye jangili wa tembo wetu na kinana ndiye kiongozi wa ccm hivyo ccm ndio majangili wa tembo wetu watanzania.
 
Nimeipata sasa hivi hii wadau, naomba tuijadili...

Na Daniel Mbega, Iringa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Sued Kagasheki, amepuliza kipenga. Kilichobaki sasa ni kwa wachezaji kushiriki kikamilifu kupambana na ujangili, kwani mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wahariri wa habari nchini iliyofanyika leo mjini Iringa, Balozi Kagasheki amesema wimbi la ujangili linazidi kuongezeka kila kukicha kiasi cha kutishia uwepo wa Tembo pamoja na viumbe wengine, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kikamilifu mapambano hayo.
“Things are rotten and should be cleaned up (mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa),” amesema Waziri Kagasheki. “Ninyi waandishi ni wachezaji katika vita hii, ingawa mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye wajibu mkubwa wa kupambana na janga hili. Mchango wa wanahabari ni muhimu sana.”
Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Balozi Kagasheki amesema, vita dhidi ya ujangili haiwezi kuonewa haya na akatoa rai kwa wanahabari kutumia taalamu yao kufichua maovu yote yanayohusiana na ujangili na kuutokomeza, vinginevyo vizazi vijavyo vitawahukumu.
Amesema vyombo vya habari visisite kuwafichua wahusika, hata kama waziri mwenyewe yumo kwenye mtandao huo, kwani maslahi ya taifa ni ya kupewa kipaumbele.
Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo, Balozi Kagasheki amesema haiyumkini kwa pembe za ndovu kukamatwa ng’ambo wakati makontena hayo yanajazwa na kusafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, hali ambayo inaleta taswira kwamba hata watumishi wa umma wanahusika kwa kiasi kikubwa.
“Pale bandarini kuna polisi, kuna customs (forodha), kuna TPA wenyewe, na kuna maofisa wa usalama. Inakuwaje basi meno haya ya tembo yanapakiwa pale na kusafirishwa, halafu yanakwenda kukamatwa Hong Kong, au Philippines, au Vietnam. Hapa kuna tatizo, lazima tuliseme,” amesema.
Amesema rushwa kwa watumishi wa umma na waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hizo ni kubwa, hali inayoifanya vita hiyo kuwa ngumu.
Hata hivyo, amesema kuongezeka kwa ujangili kunachangiwa na mambo mengi, yakiwemo mahitaji ya meno ya tembo ulimwenguni, faida itokanayo na biashara hiyo kuwa kubwa, umaskini wa wananchi, na mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa umma.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, amesema pamoja na vita hiyo kuwa ya muda mrefu, lakini inakuwa vigumu kwa vile wahusika ni watu wenye fedha na hawaogopi kupoteza chochote.
Amesema wanahabari wanatakiwa kutokuwa waoga hata kama wanaopambana nao ni watu wenye fedha.
“Msiogope hata kama hawa wana mapesa, vita hii ni kubwa na tunapaswa kupiganwa kwa nguvu zote kuhakikisha tunatetea maliasili ya taifa,” amesema.
Hata hivyo, amepinga takwimu za TAWIRI kuhusu idadi ya tembo wanaouawa kila siku na kusema mara nyingi takwimu hizo zinatengenezwa na maofisa kuilinda serikali huku katika uhalisi tatizo hilo likionekana kuwa kubwa zaidi.
“Hizi takwimu siyo sahihi na zaidi zimejikita kwenye maeneo yale tu yaliyo chini ya hifadhi, vipi kuhusu maeneo mengine ambayo hayatambuliki? Kwa hiyo, idadi ya tembo wanaouawa kila siku inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko tunavyoelezwa,” amesema.
Lembeli amesema Idara ya Maliasili haina watumishi wa kutosha, bajeti ni ndogo na maslahi ni duni, hivyo kuitaka serikali, kama kweli imedhamiria kukabiliana na tatizo hilo, basi iongeze watumishi na kuwamotisha.
Amewataka wahariri hao wa habari kuunda Jukwaa la Marafiki wa Big Five (Friends of the Big Five) litakalowashirikisha wadau mbalimbali kuanzisha mijadala ya namna ya kupambana na ujangili pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, ameitaka serikali kuongeza kasma kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kama ilivyofanya katika sekta ya madini miaka kadhaa iliyopita.
“Sekta ya madini ilitengewa fedha nyingi zaidi, lakini hivi sasa wametuachia mashimo. Sasa ni wakati wa serikali kuitengea fedha nyingi idara ya utalii na maliasili kwa sababu kuna uhakika wa kuongezeka maradufu kwa pato la taifa kutoka asilimia 17 ya sasa,” alisema.

Daniel Mbega ni Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la DARAJA LETU, ambalo ni la Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

mara baada ya semina ndefu kama hizi inafaa kujiburudisha na KINANA LAGER au KINANA LIGHT!

na hiyo ndiyo tofauti ya rwanda na tanzania...huku kwetu kila mtu ni mlalamikaji - mpaka viongozi
 
Mzee Sitta ni kulalamika,Kagasheki kulalamika sasa ni serikari ya chama gani?maccm bana?balaa tupu
 
Kaga. . . . acha utani wako bana, ina maana kinana kaingia chimbo la kufa hajulikani alipo?
 
Wanaongea sana, hakuna maamuzi yoyote wanayochukua!
 
Huyu kagesheki ni mpuuzi tu, kwa hajui kwamba kinana ndio anayeua hao tembo?...
 
Inabidi aongee hivyo kwa vile kila kitu kiko wazi, tatizo ni kwamba hana anachoweza kufanya and it will continue to get rotten further and further iwapo magamba wataendelea kutawala
 
Nimeipata sasa hivi hii wadau, naomba tuijadili...

Na Daniel Mbega, Iringa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Sued Kagasheki, amepuliza kipenga. Kilichobaki sasa ni kwa wachezaji kushiriki kikamilifu kupambana na ujangili, kwani mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wahariri wa habari nchini iliyofanyika leo mjini Iringa, Balozi Kagasheki amesema wimbi la ujangili linazidi kuongezeka kila kukicha kiasi cha kutishia uwepo wa Tembo pamoja na viumbe wengine, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kikamilifu mapambano hayo.

“Things are rotten and should be cleaned up (mambo yameoza na yanahitaji kusafishwa),” amesema Waziri Kagasheki. “Ninyi waandishi ni wachezaji katika vita hii, ingawa mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye wajibu mkubwa wa kupambana na janga hili. Mchango wa wanahabari ni muhimu sana.”

Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Balozi Kagasheki amesema, vita dhidi ya ujangili haiwezi kuonewa haya na akatoa rai kwa wanahabari kutumia taalamu yao kufichua maovu yote yanayohusiana na ujangili na kuutokomeza, vinginevyo vizazi vijavyo vitawahukumu.

Amesema vyombo vya habari visisite kuwafichua wahusika, hata kama waziri mwenyewe yumo kwenye mtandao huo, kwani maslahi ya taifa ni ya kupewa kipaumbele.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo, Balozi Kagasheki amesema haiyumkini kwa pembe za ndovu kukamatwa ng’ambo wakati makontena hayo yanajazwa na kusafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, hali ambayo inaleta taswira kwamba hata watumishi wa umma wanahusika kwa kiasi kikubwa.

“Pale bandarini kuna polisi, kuna customs (forodha), kuna TPA wenyewe, na kuna maofisa wa usalama. Inakuwaje basi meno haya ya tembo yanapakiwa pale na kusafirishwa, halafu yanakwenda kukamatwa Hong Kong, au Philippines, au Vietnam. Hapa kuna tatizo, lazima tuliseme,” amesema.

Amesema rushwa kwa watumishi wa umma na waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hizo ni kubwa, hali inayoifanya vita hiyo kuwa ngumu.

Hata hivyo, amesema kuongezeka kwa ujangili kunachangiwa na mambo mengi, yakiwemo mahitaji ya meno ya tembo ulimwenguni, faida itokanayo na biashara hiyo kuwa kubwa, umaskini wa wananchi, na mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa umma.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, amesema pamoja na vita hiyo kuwa ya muda mrefu, lakini inakuwa vigumu kwa vile wahusika ni watu wenye fedha na hawaogopi kupoteza chochote.

Amesema wanahabari wanatakiwa kutokuwa waoga hata kama wanaopambana nao ni watu wenye fedha.“Msiogope hata kama hawa wana mapesa, vita hii ni kubwa na tunapaswa kupiganwa kwa nguvu zote kuhakikisha tunatetea maliasili ya taifa,” amesema.

Hata hivyo, amepinga takwimu za TAWIRI kuhusu idadi ya tembo wanaouawa kila siku na kusema mara nyingi takwimu hizo zinatengenezwa na maofisa kuilinda serikali huku katika uhalisi tatizo hilo likionekana kuwa kubwa zaidi.

“Hizi takwimu siyo sahihi na zaidi zimejikita kwenye maeneo yale tu yaliyo chini ya hifadhi, vipi kuhusu maeneo mengine ambayo hayatambuliki? Kwa hiyo, idadi ya tembo wanaouawa kila siku inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko tunavyoelezwa,” amesema.

Lembeli amesema Idara ya Maliasili haina watumishi wa kutosha, bajeti ni ndogo na maslahi ni duni, hivyo kuitaka serikali, kama kweli imedhamiria kukabiliana na tatizo hilo, basi iongeze watumishi na kuwamotisha.

Amewataka wahariri hao wa habari kuunda Jukwaa la Marafiki wa Big Five (Friends of the Big Five) litakalowashirikisha wadau mbalimbali kuanzisha mijadala ya namna ya kupambana na ujangili pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, ameitaka serikali kuongeza kasma kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kama ilivyofanya katika sekta ya madini miaka kadhaa iliyopita.

“Sekta ya madini ilitengewa fedha nyingi zaidi, lakini hivi sasa wametuachia mashimo. Sasa ni wakati wa serikali kuitengea fedha nyingi idara ya utalii na maliasili kwa sababu kuna uhakika wa kuongezeka maradufu kwa pato la taifa kutoka asilimia 17 ya sasa,” alisema.

Daniel Mbega ni Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la DARAJA LETU, ambalo ni la Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Usanii huu wa serikali ya ccm sijui utaisha lini. waziri anawajua MAJANGILI tena anasema wanafedha eti anataka waandishi waendelee kutobolewa macho na kuteswa wao wabaki kuwatetea MAJANGILI. jumamosi nilikuwa bar fula watu wamebadili ma jina ya bia wanaita majina ya watu eti Ni ki............... wakimaanisha Ndovu.
 
Si walishaambiwa JANGILI MKUU ni nani na kuishia kumtetea pale Bungeni? Tena JANGILI lenyewe linaua Tembo na kusafirisha lenyewe! Sasa anacho taka wananchi wafanye ni nini?

Amesha kiri kwamba pamoja na taarifa mwisho wa siku serikali ndiyo inachukuwa hatua. awaambie waTnaganyika ni hatua gani wamezichukuwa kulishughulikia hilo JANGILI?

Vinginevyo wakubali tu kwamba MAGAMBA ni wabia kwenye hiyo biashara.

MSHIKWA NA NGOZI NDIYE MUIBA NG'OMBE.

Sielewi kwa nini JF mobile haina kidude cha LIKE.any way pokea like kokote kule uliko.
 
Huyu kagesheki ni mpuuzi tu, kwa hajui kwamba kinana ndio anayeua hao tembo?...

Kabla hajaanza kulalamika anapaswa auelezee umma wa Watanganyika ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya wale walioruhusu ndege ua vita ya Qatar kuondoka na twiga. Kisha aseme amechukuliwa hatua gani yule aliyepewa uwaziri and within a very short time akanunua nyumba ya $700m. Akimaliza aseme ile meli iliyokamatwa na pembe za ndovu iko wapi? Mwisho anawahakikishiaje waandishi wa habari watakaofichua ufisadi usalama wao?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ccm kuna ugonjwa wa kufisha. Wanalalamika bila kuchukua hatua yoyote sijui kwa nini? Walishaambiwa jangili nambali wani ni Kinana, sasa Kagasheki anataka waandishi wa habari waseme nini zaidi?
Kuwa ndani ya ccm ni kujiua kiroho, kiakili, na nafsi; unabaki lidude tu lisilotumia hata akili yake kufikiri.
Mfano: Mwigulu ni graduate wa uchumi daraja ya kwanza = amezama kwenye ccm sasa hakuna cha uchumi wa nini, amebakiza kufikiria juu ya kumwaga damu za watu tu. Poor ccm.
 
Back
Top Bottom