Leo kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi Startv Kafulila nimewambia watazamaji kwamba ukata wa pesa mtaani sio sababu wa kukatika kwa pesa za dili tu. Bali tatizo ktk usimamizi wa uchumi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Bank Kuu ya robo mwaka, kuanzia Juni 2016 -Septemba 2016, Ujazo wa fedha kwenye uchumi uliongezeka kwa 913bn wakati kipindi kama hicho mwaka 2015 ujazo uliongezeka kwa zaidi ya 3000bn. Yaani ujazo wa fedha mwaka 2015 ulikuwa zaidi ya mara3 ya mwaka 2016.
Na Ripoti hiyo ya BOT( quartely economic review Juni-Sept2016), imesema sababu ni kukosekana mikopo kwa sekta binafsi nchini. sasa sekta binafsi duniani kote ndio injini ya uchumi, na inaendeshwa kwa kukopa bank, kama mikopo kwa biashara inaporomoka kiasi hicho unajengaje uchumi? mikopo ya biashara sio pesa za dili.
Ni halali kwa ajili ya biashara halali. Sasa uamuzi wa sasa kwamba serikali inataka kukopa bank za ndani kiasi cha 1200bn baada ya kukosa mikopo huko Ulaya , utazidisha ukata mifukoni kwasababu hatua hiyo itasababisha bank za ndani kuzidi kupunguza mikopo kwa biashara za ndani na kuzorotesha biashara na hivyo mzunguko wa fedha kuzidi kupungua( economic austerity). Huo ndio ukweli kuhusu kwanini mtaani hakuna pesa.
Nini cha kufanya?
Serikali iongeze ujazo wa fedha kwenye uchumi hata kwa dhana ya stimulus package (ambapo serikali inaweza kutenga kiasi kikubwa cha kulipa deni kubwa la ndani na miradi yenye kugusa watu wengi). Ni utaratibu wa kawaida kwa nchi mbalimbali duniani, na Tanzania tuliwahi fanya japo kwa kasoro nyingi mwaka 2008, ambapo ilitenga kiasi cha 1.7trilion kukabili athari za mdororo wa uchumi duniani, ili kuchangamsha biashara walau tufikie kiasi cha mwaka 2015.
Ni kweli ikiongeza ujazo huo wa fedha mfumko wa bei utaongezeka lakini inafahamika kwamba mwaka 2015 pamoja na ujazo huo wa fedha kwenye uchumi mfumko wa bei ulikuwa asilimia6.3% ukilinganisha na mfumkonwa bei wa 4.8% kwa kipindi cha Juni mpaka Septemba 2016, kiasi cha 6% ni kidogo ( kwenye uchumi wanaita moderate inflation),na kinahimilika na faida zake ni nyingi kwa nchi kwasababu inachangamshara biashara na serikali inaongeza mapato ya kodi.
Chanzo: STAR TV